Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Aprili 2024

15:55:46
1450467

Uhispania kunzisha kampeni ya kutambuliwa rasmi taifa la Palestina, Australia inazingatia hatua hiyo

Serikali ya Uhispania imetangaza kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo Pedro Sanchez atakutana na baadhi ya viongozi wenzake katika Umoja wa Ulaya wiki ijayo kujaribu kuunga mkono suala la kutambuliwa rasmi taifa la Palestina.

Haya yanajiri huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Australia ikitangaza kuwa Canberra itazingatia kadhia ya kulitambua taifa la Palestina, jambo linalotambuliwia kuwa ni mabadiliko katika sera ya nchi hiyo.

Msemaji wa Serikali ya Uhispania, Pilar Alegria, amewaambia waandishi wa habari kwamba ajenda ya Sanchez inajumuisha mikutano na mawaziri wakuu wa Norway, Ireland, Ureno, Slovenia na Ubelgiji, na inaangazia msimamo wa Umoja wa Ulaya kuhusu vita vya Isarel katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.

Alegria ameongeza kuwa: "Tunataka kusitisha maafa ya binadamu huko Gaza na kusaidia kuanzisha mchakato wa amani wa kisiasa ambao utapelekea kupatikana suluhisho la serikali mbili haraka iwezekanavyo."

Awali Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez alisema kwamba anatarajia Madrid kulitambua taifa la Palestina ifikapo Julai mwaka huu, akiongeza kuwa anaamini hivi karibuni kutakuwa na "kambi muhimu" ndani ya Umoja wa Ulaya kushinikiza wanachama wengi kuchukua msimamo huo.

Msimamo huo unafuatia ukatili na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Isarel dhidi ya watu wa Gaza huko Palestina.

342/