Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Aprili 2024

15:56:16
1450468

Waislamu katika nchi mbalimbali washerehekea Idul Fitr mwishoni mwa Ramadhani

Waislamu katika maeneo mbalimbali ya dunia leo wameanza kusherehekea sikukuu ya Idul Fitr inayoadhimishwa baada ya kukamilika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sherehe za Idi zinatanguliwa na Swala ya Idul Fitr kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukamilisha ibada hiyo adhimu katika dini ya Uislamu.

Mjini Tehran Swala ya Idi imeongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei katika uwanja wa Swala wa Imam Khomeini. Ibada hiyo imehudhuriwa na umati mkubwa wa watu na baada ya Swala Ayatullah Khamenei amehutubia waumini waliopata taufiki ya kushiriki katika ibada hiyo.Katika khutba ya kwanza ya Swala hiyo Ayatullah Khamenei ameupongeza Umma wa Kiislamu na wananchi wa Iran kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul-Fitr na kuitaja Ramadhani kuwa ni mwezi wa rehma za Mwenyezi Mungu. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kislamu amewashauri Waislamu hasa vijana kutunza tunu za kiroho za mwezi wa Ramadhani. Pamoja na Iran, baadhi ya nchi zilizoanza sherehe za Idul Fitr leo ni Saudi Arabia, Uturuki, Yemen, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri, Algeria, Bahrain, Iraq, Kuwait, Palestina, Lebanon, Syria, Tunisia, Senegal, Sudan, Burkina Faso, Ivory Coast, Tanzania, Kenya, Rwanda na Mauritania. Idhaa ya Kiswahili, Redio Tehran, inawapa Waislamu wote mkono wa heri na salamu za Idi ikiwatakia nyote hususan wasikilizaji wetu sikukuu njema, na kumuomba Mola Karima atakabali dua na ibada zetu katika mwezi uliomalizaka jana wa Ramadhani. 

342/