Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Aprili 2024

15:56:50
1450469

Wafanyikazi wa Google walalamikia kandarasi ya dola bilioni 1.2 na Israel

Idadi kubwa inayozidi kungezeka ya wafanyakazi wa shirika la kiteknolojia la Google wamejiunga na kampeni ya malalalmiko ya kuitaka kampuni hiyo ya Marekani kuachana na kandarasi ya dola bilioni 1.2 inayoipatia Israel huduma za kitekonolojia zinazojulikana kama Project Nimbus.

Habari za hivi majuzi za jarida la Time zinaangazia ongezeko la ushawishi wa kampeni ya No Tech For Apartheid, yaani 'Hakuna Teknolojia kwa Apathaidi', kundi la wanaharakati ambao wamechukua msimamo dhidi ya ushirikiano wa Google na utawala wa kibaguzi na utendao jinai wa Israel, na sasa takriban wafanyakazi 40 wa Google ni miongoni wanaharakati wa kampeni hiyo.

Wiki iliyopita, Eddie Hatfield, mhandisi wa programu ya Google Cloud mwenye umri wa miaka 23, alisimama kwenye Mind the Tech, mkutano wa kila mwaka wa kukuza tasnia ya teknolojia ya Israel, na kutoa nara isemayo "Mimi ni mhandisi wa programu ya Wingu la Google, na ninakataa kutengeneza teknolojia ambayo inatia nguvu mauaji ya kimbari, ubaguzi wa rangi au ujasusi wa raia!”

Aliungwa mkono na vikundi vya Mayahudi wanaopinga Uzayuni vya Shoresh na Sauti za Kiyahudi kwa Ajili ya Amani.

Wafanyakazi wawili wa Google pia hivi karibuni walitangaza kujiuzulu kutoka kwenye kampuni hiyo kubwa ya teknolojia kutokana na kuhusika kwake katika jitihada za pamoja za mradi wa dola bilioni 1.2  kati ya Google na Amazon wa kutoa huduma za Akili Mnemba au AI kwa jeshi katili la Israel.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alikemea hatua ya utawala haramu wa Israel kutumia Akili Mnemba au Artificial Intelligence (AI) kwenye vita dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Wataalamu wanasema, matumizi ya Akili Mnemba vitani huko Gaza ni chanzo cha kuuawa kiholela idadi kubwa ya raia, hasa wanawake na watoto.

342/