Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Aprili 2024

15:57:19
1450470

Kansela wa Ujerumani ashinikizwa kuacha kuipatia Israel silaha

Mamia ya watumishi wa umma wa Ujerumani wameungana na harakati ya kumtaka Kansela Olaf Scholz aache kuupatia silaha utawala haramu wa Israel huku utawala huo ukiendeleza jinai zake za kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Takriban wafanyikazi waandamizi 600 wa sekta ya umma walimwandikia barua Scholz siku ya Jumatatu, wakimtaka yeye na maafisa wake wakuu "kukomesha utumaji wa silaha kwa Israeli mara moja."

"Israel inafanya uhalifu huko Gaza ambao unakinzana waziwazi na sheria za kimataifa", imesema sehemu moja ya barua hiyo.

Kundi hilo limenukuu uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki mnamo Januari ambayo ilisema mashambulizi ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza ni sawa na "vitendo vinavyoweza kutajwa kuwa ni mauaji ya kimbari."

Kesi hiyo ilifikishwa katika mahakama ya dunia, iliyoko The Hague, dhidi ya utawala wa Afrika Kusini mwezi Desemba.

Nicaragua pia imeifikisha Ujerumani mbele ya mahakama hiyo ya kiimataifa kuwataka majaji watoe hukumu ya hatua za dharura kuizuia Berlin kuipatia Israel "silaha na misaada mingine."

Wanasheria wa Nicaragua wamesema kuwa, Ujerumani inawezesha mauaji ya kimbari huko Gaza kwa kuupa silaha utawala wa Tel Aviv.

Mashinikizo ya kimataifa yanazidi kuongezeka kwa Ujerumani na Marekani kusitisha upelekaji silaha kwa Israel huku vita vya mauaji ya kimbari vya utawala huo vikiendelea kwa muda wa miezi sita katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa, na zaidi ya Wapalestina 33,300 wakiuawa hadi sasa, wengi wakiwa ni wanawake na watoto.

Ujerumani na Marekani zinatuma takriban asilimia 99 ya silaha zote zinazoingizwa Israel; hayo ni kulingana na uchambuzi uliochapishwa Machi na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI).

342/