Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Aprili 2024

19:25:00
1450812

Haaretz: Serikali ya Netanyahu imeshindwa vibaya kwenye vita vya Ghaza

Chombo kimoja cha habari cha utawala wa Kizayuni kimekiri kwamba Wazayuni wote wanakiri kuwa serikali ya Benjamin Netanyahu imeshindwa vibaya kwenye vita vya Ghaza.

Shirika la habari la Mehr limelinukuu gazeti hilo la Kizayuni likifichua kwamba, ukitoa Wazayuni wanaojifanya vipofu, Wazayuni wengine wote wanakiri kuwa Israel imepata pigo na imeshindwa vibaya kwenye vita vya Ghaza.

Katika sehemu moja ya ripoti yake hiyo gazeti la Kizayuni la Haaretz limeandika: Hatukupaswa kusema haya, lakini hatuna njia nyingine. Sisi tumeshindwa vitani, tumeshindwa kikamilifu. 

Mwandishi wa makala hiyo amesisitiza kuwa, Wazayuni wanajaribu kujibabaisha kwa kuonesha hawajakula kipigo kwenye vita hivyo kwani ni uchungu sasa kukubali uhakika huo wa mambo. 

Kabla ya hapo tovuti maarufu ya Kizayuni ya Walla! ilikuwa imetangaza kuwa, madai kwamba Israel imepata ushindi mutlaki ni bwabawaja na upayukaji usio na chochote ndani. Uzoefu mchungu wa wanajeshi wa Israel hasa katika mapigano ya nchi kavu unathibitisha kuwa Wapalestina muda wote ndio washindi.

Gazeti la Kizayuni la Haaretz limeripoti pia kuwa, jeshi la Israel limelazimika kuondoa wanajeshi wake katika mji wa Khan Yunis huko Ghaza bila ya kufanikisha malengo yake makuu.

342/