Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Aprili 2024

19:25:30
1450813

UN: Israel inaichezea tu misamiati kama "ngao ya binadamu" na "maeneo yenye usalama"

Ripota wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesisitiza kuwa, viongozi wa utawala wa Kizayuni na askari wa utawala huo wanapotosha na wanaichezea misingi ya sheria za kimataifa ili kuhalalisha ukatili na uchokozi wao.

 ametoa wito wa kupigwa marufuku uuzaji wa silaha kwa Israel na kuwekewa vikwazo vya kiuchumi utawala huo dhalimu na ghasibu. Albanese amesema: utawala wa Kizayuni lazima ushinikizwe ili uheshimu sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Ripota huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ameongeza kuwa: hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa kufanya jinai za kivita katika miaka ya nyuma.Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi, utawala wa Kizayuni umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina, na kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za haki za binadamu mbele ya jinai za Israel zimepelekea kuendelezwa mauaji ya wanawake na watoto Palestina yanayofanywa na utawala huo. Idadi ya mashahidi wa vita huko Gaza imepindukia, elfu 33,175 na idadi ya waliojeruhiwa imeongezeka na kupindukiza 75,886.

 Baada ya kupita miezi sita tangu utawala wa Kizayuni uivamie Ghaza bila ya kupata matokeo na mafanikio yoyote, utawala huo unazidi kuzama kwenye kinamasi cha migogoro ya ndani na nje siku baada ya siku. Katika kipindi hiki, utawala wa Kizayuni haujapata mafanikio yoyote isipokuwa ya kufanya jinai, mauaji ya halaiki, uharibifu, jinai za kivita, ukiukaji wa sheria za kimataifa, kushambulia mashirika ya misaada na kuliweka eneo la Ghaza kwenye njaa na mateso.../

 


342/