Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Aprili 2024

19:26:08
1450814

Imamu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Utawala wa Kizayuni unakaribia kutoweka

Imamu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amelaani mauaji na jinaii zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na kusema: Utawala huo unaelekea kuporomoka.

Hujjatul Islam wa Muslimin Kazem Seddiqi ameyasema hayo katika hotuba za Swala ya Ijumaa hii leo mjini Tehran na kubainisha kuwa, Gaza ndio kadhia nambari moja ya Umma wa Kiislamu. Ameeleza kuwa subira, kujitoa mhanga na mapambano ya watu wa Gaza yamefika kileleni na kusema: Watu wa Gaza wametoa zaidi ya mashahidi elfu 33 na bado wanapigana kijasiri na utawala bandia wa Israel.

Amesisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni umenaswa katika mtego ambao umeutengeneza wenyewe na hauna njia ya kuuepuka, na mwishowe utaangamizwa.

Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amezikosoa serikali za nchi za Waislamu kwa kutotekeleza matakwa ya wananchi ya kukata uhusiano na utawala haramu wa Israel na kuongeza kuwa: Licha ya mapambano, kujitolea mhanga na ushujaa wa wanamapambano ya ukombozi wa Palestina, lakini serikali za nchi za Waislamu hazitimizi majukumu yao, na Marekani na Ulaya zinaendelea kuusaidia utawala wa Kizayuni wa Israel unaoua watoto na wanawake.

Zaidi ya Wapalestina elfu 33 wameuawa na wengine zaidi ya elfu 75 wamejeruhiwa na kufanywa vilema katika mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Isrel Ukanda wa Gaza, huko Palestina.

342/