Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Aprili 2024

19:26:40
1450815

Raisi: Madola ya kibeberu yanazusha fitna ili kuvuruga usalama kati ya Iran na Pakistan

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kustawishwa uhusiano wa Iran na Pakistan hakufurahishi madola ya kibeberu na kwa hivyo yanazusha fitna ili kuleta mpasuko kati ya mataifa hayo mawili na nchi hizo mbili za Kiislamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la wanachuo wa Iran (ISNA), Sayyid Ebrahim Raisi ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan, ambapo alieleza kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni wa kina, wa kihistoria na unaozingatia masuala mengi ya pamoja yasiyoweza kutenganika katika nyanja za dini, imani, utamaduni na ujirani na akaongezea kwa kusema, anatumai kuwa katika kipindi kipya, uhusiano wa pande mbili utastawishwa zaidi kwa ajili ya kudhamini maslahi ya mataifa hayo mawili.Raisi amepongeza imani na ghera iliyoonyeshwa na vijana wa Umma wa Kiislamu katika kuondoa fitna mbalimbali ikiwemo ya tapo la kigaidi la DAESH (ISIS) na kusisitiza kuwa: "inapasa tuimarishe mashirikiano katika kupambana na ugaidi ili kuzuia kufikiwa takwa la maadui na vilevile kustawishwa urafiki uliopo kati ya Tehran na Islamabad".

Katika sehemu nyingine ya mazungumzo hayo,  Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kuendelea jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza ni majonzi makubwa kwa nchi za Kiislamu na watetezi wote wa uhuru duniani na akasisitizia udharura wa kufanywa juhudi za pamoja na nchi zenye misimamo uhuru na zisizo na utegemezi ili kutoa mashinikizo athirifu kwa ajili ya kukomesha jinai za utawala huo unaoteketeza roho za watoto.

Kwa upande wake, Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan mbali na hujuma ya kigaidi iliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika sehemu ya ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus, Syria amesema: mfanano mkubwa uliopo wa kitamaduni na kistaarabu kati ya Iran na Pakistan unaandaa mazingira mwafaka ya kupanuliwa na kustawishwa uhusiano wa kitamaduni, kibiashara na kiuchumi na mabadilishano ya uwezo na fursa nyingi na tofauti zilizoko katika mataifa haya mawili.

Uhusiano wa Iran na Pakistan una historia ndefu ya tangu enzi za uhuru wa Pakistan na katika miaka ya hivi karibuni uhusiano wa Tehran na Islamabad umekuwa ukiongezeka zaidi katika sekta mbalimbali.../

342/