Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Aprili 2024

19:27:05
1450816

Mwakilishi wa Iran UN asisitiza ulazima wa kuuadhibu utawala vamizi wa Israel

Ofisi ya Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa imesema Baraza la Usalama lilipaswa kulaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo ya kidiplomasia ya Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria.

Jumatatu Aprili Mosi, ndege za kijeshi za Israel zilishambulia sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria na kuuwa shahidi washauri saba wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu. Miongoni mwa waliouawa shahidi ni Jenerali Mohammad Reza Zahedi na Jenerali Mohammad Hadi Haj Rahimi pamoja na watu wengine watano waliokuwa pamoja nao.

Katika ujumbe kupitia ukurasa wa kijamii wa X, Ofisi ya Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa imesema:  "Iwapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lingelaani kitendo cha uchokozi cha utawala wa Kizayuni dhidi ya majengo yetu ya kidiplomasia huko Damascus na baadaye kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wa hujuma hiyo, sharti la Iran la kuuadhibu utawala huo mbovu lingeweza kuondolewa."

Viongozi wa Iran wameahidi kulipiza kisasi kufuatia jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wiki iliyopita, Marekani, Uingereza na Ufaransa zilipinga taarifa rasmi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na Russia ambayo ingelaani shambulio hilo.

342/