Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Aprili 2024

19:27:30
1450817

Amir Abdollahian: Kujilinda kwa lengo la kumuadhibu mchokozi ni jambo la lazima

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kislamu ya Iran amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unapokiuka kikamilifu kinga ya watu binafsi na maeneo ya kidiplomasia kwa kukanyaga sheria za kimataifa na Mikataba ya Vienna, inakuwa lazima kujihami kwa lengo la kumuadhibu mchokozi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdollahian, aliyasema hayo jana Alhamisi katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Analena Berbuk. Aligusia shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, ambalo liliuwa shahidi washauri saba wa kijeshi wa Iran na kuongeza kuwa, sera ya mambo ya nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima ni kuepusha mivutano.

Amir Abdollahian amesema matarajio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuona Ujerumani ikilaani jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel, na kuongeza kuwa, Israel ni utawala vamizi na Palestina ina haki ya kujihami. Katika mwelekeo huu, njia pekee ya kutatua matatizo ya sasa ni kukomesha mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita katika Ukanda wa Gaza.

Waziri wa Mambo ya je wa Iran amesema kuwa, sababu iliyopelekea juhudi za Ujerumani za kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Gaza zishindwe kufanikiwa, ni msimamo wa Berlin wa kuegemea upande mmoja katika mauaji ya kimbari ya utawala ghasibu wa Israel.

Kwa upande wake Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ujerumani amempongeza mwenzake wa Iran kwa mnasaba wa Sikukuu ya Idul Fitr na kusisitiza kuwa, sikukuu hiyo ni mjumbe wa amani.

Kuhusu shambulio la utawala wa Israel kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Annalena Baerbock amesisitiza kuwa maeneo ya kidiplomasia yana kinga kamili.

342/