Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

12 Aprili 2024

19:27:59
1450818

Euro-Med: Zaidi ya Wapalestina 13,000 hawajulikani waliko tangu vilipoanza vita vya Ghaza hadi sasa

Shirika la kutetea haki za binadamu la Euro-Mediterranean Human Rights Watch limetangaza kuwa Wapalestina zaidi ya 13,000 wametoweka na hawajulikani waliko tangu vilipoanza vita katika Ukanda wa Ghaza hadi sasa.

Kwa mujibu wa chaneli ya habari ya Russia Al-Yaum, Euro-Mediterranean Human Rights Watch imetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa za kupeleka vifaa maalumu na timu maalumu za wataalamu huko Ghaza ili kuondoa vifusi vya nyumba na majengo yaliyoharibiwa katika mashambulizi ya kinyama ya jeshi la Kizayuni na vilevile kuokoa maisha ya watu waliobaki chini ya vifusi pamoj na kuvitoa viwiliwili vya waliouawa shahidi. Aidha, shirika hilo la kutetea haki za binadamu limetilia mkazo ulazima wa kutolewa mashinikizo makubwa ya kimataifa kwa utawala wa Kizayuni ili kuhakikisha unadhamini usalama wa wafanyakazi wa utoaji misaada na wale wanaoondoa vifusi vikiwemo vikosi vya ulinzi wa raia na kujulikana hatima ya maelfu ya Wapalestina waliotoweka katika eneo la Ukanda wa Ghaza, ambao walitiwa nguvuni na vikosi vya jeshi la utawala huo.

Kwa mujibu wa tangazo la Wizara ya Afya ya Palestina, katika kipindi cha saa 24 zilizopita, jeshi la utawala wa Kizayuni limefanya mauaji kadhaa katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza na kupelekea Wapalestina zaidi ya 89 kuuawa shahidi na wengine 120 kujeruhiwa.

 Kwa mujibu wa wizara hiyo, Wapalestina 33,634, wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameshauliwa shahidi hadi sasa na wengine 76,214 wamejeruhiwa tangu utawala haramu wa Israel ulipoanzisha vita vya kinyama na mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Ghaza Oktoba 7,2023.../


342/