Main Title

source : Parstoday
Jumapili

14 Aprili 2024

19:30:20
1451294

Tangu Oktoba 7, jeshi la Israel limefanya mauaji 16 ya halaiki kila siku katika Ukanda wa Ghaza

Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limefanya kwa wastani, mauaji 16 ya halaiki kila siku katika Ukanda wa Ghaza tangu Oktoba 7, 2023 ambako limekuwa likiendesha vita vya kinyama vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo kwa mwezi wa sita sasa.

Ofisi ya Vyombo vya Habari ya serikali ya Ghaza imetoa taarifa maalumu ikielezea kwa kina mashambulio ya siku 190 yaliyofanywa na jeshi la Kizayuni huko Ghaza. Taarifa hiyo imesema, jeshi la Israel limefanya "mauaji 2,973 katika Ukanda wa Ghaza tangu Oktoba 7, 2023."Kwa mujibu wa ripoti ya taarifa hiyo katika mashambulizi hayo ya kinyama yaliyofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, watoto 14,560 na wanawake 9,582 wameuawa shahidi.Mbali na hayo, watu 7,000 wamekwama chini ya vifusi au hawajulikani waliko, huku hospitali zikipokea jumla ya watu 33,686 waliouawa na 76,309 waliojeruhiwa.

Imeelezwa pia kuwa asilimia 72 ya waathirika wa mashambulizi ya jeshi la Kizayuni huko Ghaza ni wanawake na watoto. Taarifa hiyo aidha imebainisha kuwa huko Ukanda wa Ghaza, ambako hatua za Israel zimesababisha janga la njaa, imejitokeza hali mbaya sana ya kibinadamu kutokana na utawala wa Kizayuni kuzuia misaada isiingizwe katika eneo hilo. Kutokana na hali hiyo, watoto 30 wamefariki dunia kutokana na utapiamlo na upungufu wa maji mwilini.Taarifa hiyo ya vyombo vya habari vya Serikali ya Ghaza imeendelea kueleza kuwa jeshi la utawala haramu wa Israel limedondosha zaidi ya tani 70,000 za mada za miripuko huko Ghaza tangu Oktoba 7 hadi sasa, zikilenga sio tu maeneo ya raia bali pia sekta ya afya.../

342/