Main Title

source : Parstoday
Jumanne

16 Aprili 2024

18:24:44
1451861

Vyombo vya habari vyafichua jinai ya Wazayuni katika Hospitali ya al-Shifa huko Gaza

Vyanzo vya habari vimevichua na kuweka wazi jinai kubwa iliyofanywa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Hospitali ya al-Shifa huko Gaza baada ya kufukuliwa miili ya mashahidi wa Kipalestina waliouawa na kuzikwa na wanajeshi wa utawala huo haramu.

Televisheni ya Al-Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, vikosi vya uokoaji vya Gaza vimegundua idadi kubwa ya miili ya Wapalestina iliyozikwa kwenye vifusi vya udongo karibu na Hospitali ya al-Shifa.

Kwa mujibu wa Ismail al-Thwabateh, Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya Serikali ya Ukanda wa Gaza, utawala wa Israel umewaua shahidi Wapalestina 400 katika Hospitali ya al-Shafa.