Main Title

source : Parstoday
Jumanne

16 Aprili 2024

18:29:14
1451869

Mienendo ya chuki dhidi ya Uislamu yaongezeka nchini Ujerumani

Vyombo vya habari vya Ujerumani, vimenukuu ripoti zilizochapishwa na serikali ya nchi hiyo, na kuripoti kuwa uhalifu dhidi ya Waislamu nchini humo uliongezeka mwaka 2023 ikilinganishwa na miaka ya kabla yake.

Shirika la Habari la Ujerumani (DPA), limenukuu jibu la serikali kwa uchunguzi wa mbunge wa Christian Democratic Union (CDU) Christoph de Vries,  na kuripoti kuwa mwaka 2023, takribani vitendo 1,464 vya ukatili dhidi ya Waislamu vilirekodiwa nchini humo, ikilinganishwa na mwaka uliopita (610) na kwamba takwimu hizo zinaonyesha ongezeko mara mbili la chuki na hujuma dhidi ya Waislamu.Awali, polisi wa Ujerumani walikuwa wamechapisha ripoti ya kesi za uhalifu dhidi ya Waislamu, ambazo idadi yake ilifikia 137 katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu. Polisi ya Ujerumani inaamini kuwa ongezeko la jinai na uhalifu dhidi ya Waislamu linahusishwa na kushadidi vita vya Ukanda wa Gaza. Tangu kuanza kwa mashambulio ya Israel katika ukanda wa Gaza, serikali ya Ujerumani imekuwa ikieleza wasiwasi wake kuhusu ongezeko la ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu nchini humo. Ikiwa na zaidi ya watu milioni 84, Ujerumani ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu katika bara la Ulaya baada ya Ufaransa. 

342/