Kamati hiyo imetangaza leo kuwa, tangu vilipoanza vita vya kinyama na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza tarehe 7 Oktoba 2023 hadi sasa, wafungwa 16 wakazi wa ukanda huo wameuawa shahidi katika jela za utawala huo kutokana na mateso. Kamati inayoshughulikia masuala ya Wapalestina wanaoshikiliwa na walioachiwa huru kutoka kwenye magereza ya Wazayuni imeongeza kuwa, licha ya wafungwa wa Kipalestina kuendelea kuteswa katika jela za utawala wa Kizayuni, dunia imeendelea kukaa kimya na kuwa kitu kimoja na utawala huo ghasibu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wananchi wa Palestina wanakabiliwa na mashambulizi na jinai za walowezi maghasibu wa Kizayuni waliojizatiti kwa silaha, wanaotekeleza moja kwa moja amri za utawala wa Kizayuni.Tangu vilipoanza vita vya Ghaza, Wapalestina wasiopungua elfu tatu wakazi wa eneo hilo wamekamatwa na jeshi la Kizayuni na kutiwa magerezani.
342/