Kwa mujibu wa IRNA, Rais Raisi ameyasema hayo leo asubuhi katika hafla ya gwaride la Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo sambamba na kutoa pongezi kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Jeshi la Iran amesema: "Jeshi liko pamoja na taifa la Iran na limejiweka tayari kikamilifu kwa ajili ya kulinda nchi, ardhi yote na tunu za Mapinduzi ya Kiislamu". Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: baada ya Kimbunga cha Al-Aqsa cha Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni, Operesheni ya Ahadi ya Kweli imeporomosha haiba ya utawala huo na kuthibitisha kuwa, nguvu zao ni za utando wa buibui tu; na nguvu na uwezo ambao Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na Jeshi zimeonyesha kulingana na amri iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu ulikuwa ni wa kuutia adabu utawala wa Kizayuni.Sayyid Ebrahim Raisi ameongezea kwa kusema: "Operesheni ya Ahadi ya Kweli ilikuwa ya kiwango maalumu na si ya pande zote. Kama ingepangwa kuchukuliwa hatua kubwa, wangeona utawala wa Kizayuni usingesalia chochote, lakini ilipangwa iwe ni hatua ya kiwango maalumu, ya kuutia adabu utawala wa Kizayuni na kuvilenga vituo vilivyochukua hatua dhidi ya Iran".
342/