Main Title

source : Parstoday
Jumapili

21 Aprili 2024

18:00:13
1453020

Mwanamke mjamzito, watoto 10 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa hivi karibuni na Israel

Jeshi katili la Israel limefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya Rafah, na kuwauwa takriban watu 16, akiwemo mama mjamzito, katika mji huo wenye msongamano mkubwa wa watu kusini mwa Gaza.

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti leo Jumapili kwamba baba, binti na mama mjamzito walipoteza maisha baada ya jeshi vamizi la Israel kulenga nyumba ya familia yao katika kambi ya al-Shaboura katikati mwa Rafah.

Mwanamke huyo mjamzito, aliyefikishwa katika hospitali ya Kuwait, alikuwa tayari amekufa, lakini madaktari waliweza kumuokoa mtoto wake ambaye alikuwa tumboni.

Rafah ni eneo lililoko katika mpaka wa kusini wa Ukanda wa Gaza uliofungwa na Misri, na hivi sasa eneo hilo ni makao ya Wapalestina wapatao milioni 1.5 ambao wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na vita vya mauaji ya halaiki vinavyoungwa mkono na Marekani katika eneo hilo.

Israel ilikuwa imedai kuwa Rafah ni "eneo salama," kwa wakimbizi lakini sasa inatishia kutekeleza mashambulizi ya kijeshi na kueneza hofu miongoni mwa wakimbizi.

Shambulio hilo la Jumapili ya leo limeongeza hofu juu ya mauaji mapya dhidi ya Wapalestina na kulaaniwa kimataifa.

Utawala katili wa Israel ulianzisha hujuma yake ya kikatili dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba na hadi sasa umewaua Wapalestina wasiopungua 34,049, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine 76,901 kujeruhiwa.

342/