Main Title

source : Parstoday
Jumapili

21 Aprili 2024

18:03:49
1453027

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran ashukuru majeshi kwa utendaji mzuri katika matukio ya hivi karibuni

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Vikosi vya kijeshi vimeonyesa taswira nzuri ya uwezo na mamlaka yao, na pia taswira yenye kupongezwa ya taifa la Iran, sambamba na kuthibitisha kuibuka kwa uwezo wa irada wa taifa la Iran katika uga wa kimataifa.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei katika kikao na makamanda wakuu wa Jeshi la Iran ametoa pongezi kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi na pia kumbukumbu ya kuasisiwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kusema: "Mafanikio ya hivi karibuni ya jeshi yameibua hisia ya utukufu kuhusu Iran ya Kiislamu mbele ya walimwengu na weledi wa mambo duniani."

Ayatullah Khamenei amepongeza kuwepo utaratibu wa mipango sahihi katika harakati za jeshi  na kusema: "Matukio mbalimbali yana gharama na faida, na ni muhimu kupunguza gharama na kuongeza faida kwa kuwepo mipango sahihi na hivi ndivyo vikosi vya kijeshi vimefanya katika matukio ya hivi karibuni."

Akishukuru juhudi na shughuli za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Jeshi la Iran (Artesh) na Jeshi la Polisi, ameshauri na kukumbusha vikosi vya kijeshi kuhusu kuendelea kufanya bidii na kusonga mbele kukabiliana na uhasama wa maadui kwa kutegemea uvumbuzi na mipango madhubuti huku akisisitiza kuwa hakupaswi kuwepo hata lahadha moja ya kusitisha jitihada kwani kusitishwa huko kuna maana ya kurudi nyuma. Kwa msingi huo kuwepo uvumbuzi katika silaha na mbinu za kivita, pamoja na kupata taarifa kuhusu mbinu za adui, ni mambo ambayo lazima yawe kwenye ajenda kila wakati.Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, adhama ya taifa la Iran inapaswa kubainishwa mbele ya walimwengu na kuongeza kuwa: "Sambamba na kutambua maafisa wenye vipaji na ubunifu, ni lazima kuwa na imani madhubuti juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuelekeza matumani Kwake na hali kadhalika kufahamu kuwa ahadi ya Mwenyezi Mungu kuhusu kuwatetea waumini ni jambo la yakini." Jumatatu, Aprili 1, 2024, utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia sehemu ya ubalozi wa Iran mjini Damascus katika shambulio la kigaidi lililopelekea kuuawa shahidi washauri saba wakuu wa kijeshi wa Iran. Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran aliitaja hatua ya Israel kuwa ni shambulio dhidi ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, utawala wa Kizayuni "utaadhibiwa". Katika kutekeleza ahadi hiyo, Jumapili asubuhi (tarehe 14 Aprili 2024), Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilichukua hatua ya kuuadhibu utawala huo wa Kizayuni kwa kuvurumisha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) kupitia operesheni ya kuiadhibu Israel iliyopewa jina la Ahadi ya Kweli."

342/