Main Title

source : Parstoday
Jumapili

21 Aprili 2024

18:04:16
1453028

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman: Vita Ukanda wa Gaza visitishwe haraka iwezekanavyo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na mwenzake wa Oman wamesisitiza juu ya haja ya kutekelezwa juhudi za kimataifa ili kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni, kufikiwa mapatano ya usitishaji vita na kutumwa haraka misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Gaza.

Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezungumza kwa simu na Seyyed Badr bin Hamad Albusaidi na kupongeza msimamo madhubuti wa serikali ya Oman kuhusu matukio ya karibuni katika eneo hili.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman pia amelaani hatua za kuyumbisha usalama za utawala wa Kizayuni katika eneo na kusistiza kuwa njia pekee ya kurejesha amani katika Mashariki ya Kati ni kukomesha jinai za kivita za utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza. 

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Oman pia wamechunguza matukio ya karibuni huko Ukanda wa Gaza na jitihada za kimataifa za kuhitimisha jinai za utawala wa Kizayuni, kufikiwa mapatano ya kusimamisha vita na kutumwa haraka misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Gaza. 

Tangu tarehe saba mwezi uliopita wa Oktoba, kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi, utawala wa Kizayuni umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina mkabala wa kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu.Hadi sasa maelfau ya raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza wameuliwa shahidi na kujeruhiwa wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.  


342/