Main Title

source : Parstoday
Jumapili

21 Aprili 2024

18:04:40
1453029

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Afrika Kusini wafanya mazungumzo kwa njia ya simu

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Afrika Kusini wamezungumza kwa njia ya simu na kujadili matukio ya hivi punde zaidi katika uhusiano wa pande mbili na hali ya eneo la Asia Magharibi, hususan baada ya jibu halali la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mashambulizi ya hivi karibuni ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni kwenye ubalozi wa Iran huko Damascus, Syria.

Katika mazungumzo hayo,  Waziri wa Mashauri ya Kigeni Iran Hossein Amir-Abdollahian amemfahamisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Bi Naledi Pandor kwamba,  kutokana na ukweli kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halikutoa jibu linalofaa kulaani hujuma ya utawala wa Israel dhidi ya ubalozi wa Iran huko Damascus na kutokana na kuwa Marekani, Uingereza na Ufaransa, ambazo ni wanachama wa kudumu wa baraza nazo pia hazikulaani jinai hiyo ya Israel Katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Iran iliamua kulenga vituo viwili vya kijeshi na kijasusi vya utawala wa Israel, vilivyohusika katika hujuma hiyo. Amesema jibu la kijeshi la Iran dhidi ya Israel lilifanyia kwa kuzingatia sheria na kanuni za kimataifa za kujihami.Amir Abdollahian ameongeza kuwa, baada ya operesheni hiyo,  alitangaza kwa jumuiya ya kimataifa ikiwemo Marekani kwamba Iran haitaki kupanua vita hivyo, lakini iwapo utawala wa Israel utachukua hatua tena dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatoa jibu lenye nguvu na shadidi.

Katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran pia amepongeza hatua ya kihistoria ya serikali ya Afrika Kusini ya kufungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutookana na mauaji yake ya kimbari huko Gaza.

Kwa upande wake, Bi Naledi Pando, amesisitiza kuhusu kusitishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza.

Ameongeza kuwa ziara ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Afrika Kusini


342/