Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

22 Aprili 2024

15:51:58
1453268

Kamanda Mwandamizi: Israel imeshindwa na Muqawama Ghaza, viongozi watamatishe vita

Yitzhak Barik, Jenerali mstaafu wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa jeshi la utawala huo haramu limeshindwa na Muqawama wa Palestina katika vita vya Ukanda wa Ghaza na kutaka viongozi wa utawala huo watangaze utamatishaji wa vita hivyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Palestina SAMA, Jenerali Barik amebainisha kuwa, malengo ya utawala haramu wa Israel yaliyopelekea kuanzisha mashambulio dhidi ya Ghaza bado hayajafikiwa na akasema, Israel inapaswa kutangaza uhitimishaji wa vita huko Ghaza. Barik ameongeza kuwa, kuivamia kijeshi Rafah, mji wa kusini mwa Ukanda wa Ghaza, hakutausaidia vyovyote utawala huo, kwa sababu Israel imeshindwa katika vita na Muqawama. Jenerali huyo mstaafu wa jeshi la utawala wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari ametamka bayana kuwa, hakuna nguvu inayoweza kuuangamiza moja kwa moja Muqawama ili usiwepo tena.

Baada ya kupita zaidi ya miezi sita tangu utawala wa Kizayuni wa Israel uivamie Ghaza bila ya kupata matunda wala mafanikio yoyote, utawala huo unazidi kuzama kwenye kinamasi cha migogoro yake ya ndani na nje siku baada ya siku.Yitzhak Barik, Jenerali mstaafu wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa jeshi la utawala huo haramu limeshindwa na Muqawama wa Palestina katika vita vya Ukanda wa Ghaza na kutaka viongozi wa utawala huo watangaze utamatishaji wa vita hivyo.

342/