Kwa mujibu wa kanali ya habari ya Al Jazeera, Brigedi za Hizbullah ya Iraq (Kataaib Hizbullah) vimetangaza katika taarifa kwamba kuanzishwa tena kwa operesheni za mashambulio dhidi ya Marekani ni matokeo ya kutopigwa hatua yoyote katika mazungumzo kuhusiana na kuondolewa majeshi ya Marekani nchini Iraq yaliyofanyika katika ziara ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mohammad Shia al- Sudani mjini Washington. Kataaib Hizbullah ni sehemu ya mtandao wa Muqawama wa Kiislamu wa Iraq, ambao mwezi Oktoba mwaka jana ulianzisha mashambulio dhidi ya vikosi vya Marekani vilivyoko Iraq na Syria ukisisitiza kuwa unafanya hivyo kujibu mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza na kupinga uwepo wa majeshi ya Marekani nchini Iraq na katika eneo. "Kilichofanyika muda mchache nyuma ni mwanzo tu", imeeleza taarifa ya Kataaib Hizbullah ikimaanisha shambulio la roketi la siku ya Jumapili lililolenga kituo cha jeshi la Marekani nchini Syria.Wiki iliyopita, Mohammad Shia al-Sudani, alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Joe Biden wa Marekani katika Ikulu ya White House wakati wa ziara yake nchini humo.
342/