Main Title

source : Parstoday
Jumatano

24 Aprili 2024

19:44:50
1453835

Mmarekani ambaye hana uraia wa Israel akiri kuua watu katika vita huko Gaza

Sami Benn, Myahudi raia wa Marekani, amekiri kwamba umeshiriki katika vita vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza kwa muda wa miezi miwili na kuua Wapalestina, bega kwa bega na jeshi la Israel.

Sami Benn amesema katika mahojiano na vyombo vya habari baada ya kurejea Marekani kwamba alihudumu katika jeshi la Israel baada ya kupata visa ya kitalii na kwenda katika maeneo yanayokaliwa ya Palestina, na kwamba alikuwa huko Oktoba 7 mwaka jana, na alipata mafunzo katika jeshi la Israel kabla ya kushiriki vitati na kuua Wapaletina.

Mmarekani huyo ameongeza kuwa mafunzo hayo yalimpa fursa ya kujiunga na jeshi la Israel tarehe 7 Oktoba.

Kushiriki kwa raia huyo wa Marekakni katika operesheni za jeshi la Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza kumezua hasira miongoni mwa watumiaji wa majukwaa ya mitandao ya kijamii, ambao baadhi wanahoji: Ni watoto wangapi umeuwa, na nyumba ngapi umelipua? Je, umeshiriki katika kuhamisha na kuharibu maisha ya familia ngapi?

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamesema Mmarekani, Sami Benn, na wengine mfano wake wanaoshirikiana na jeshi katili la Israel katika mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina, wanapaswa kufunguliwa mashtaka katika mahakama za kimataifa za uhalifu wa kivita.

Vilevile wameeleza kushangazwa na msimamo wa serikali ya Marekani wa kufumbia macho ushiriki wa baadhi ya raia wake katika mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na kutowachukulia hatua za kisheria, huku ikizuia shughuli yoyote ya wanafunzi wa vyuo vikuu inayounga mkono mapambano ya ukombozi ya Palestina.

342/