Main Title

source : Parstoday
Jumatano

24 Aprili 2024

19:50:58
1453846

Ripoti: Nusu ya watu duniani wanazama katika madeni

Ripoti mpya ya Shirika la Fedha la Maendeleo ya Kimataifa imefichua kuwa karibu nusu ya watu duniani wanaishi katika nchi ambako fedha zinazotolewa kulipa madeni zinazidi fedha za matumizi ya huduma za msingi za kijamii kkama elimu na afya.

Shirika la Red Flag, ambalo limetoa maoni kuhusu ripoti hiyo limesema: Hali hii mbaya inawakilisha "sura mbaya zaidi ya madeni tangu mwanzo wa kusajiliwa rekodi za kimataifa katika uwanja huu". Ripoti hiyo inatoa taswira mbaya ya matatizo ya kifedha yanayokumba maeneo mengi ya dunia.

Data zilizomo kwenye ripoti hiyo zinaeleza kwamba, malipo ya huduma ya deni katika nchi za kipato cha chini yameongezeka kwa kiasi kikubwa, zaidi ya mara mbili ya matumizi katika sekta ya elimu, na mara nne zaidi ya matumizi katika sekta ya afya.

Ripoti ya kila mwaka ya IMF ya 2022 inatoa picha mbaya zaidi, ikibainisha kuwa 60% ya nchi zenye kipato cha chini tayari zilikuwa zikielekea ukingoni mwa mgogoro wa madeni.

Kwa mujibu wa shirika la Red Flag, mzigo wa huduma ya deni katika sehemu ya kusini ya dunia umefikia kiwango cha kutisha cha dola nusu trilioni kila mwaka, na kuzilazimisha zaidi ya nchi 100 kupunguza matumizi katika sekta muhimu kama vile afya na elimu ili kulipa madeni.Red Flag inasema: Nchi za Kiafrika, kwa mfano, zina viwango vya riba mara 4 zaidi ya Marekani na mara 8 zaidi ya nchi za Ulaya Magharibi..

342/