Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

25 Aprili 2024

17:16:32
1454077

Rais wa Ureno asema inawapasa "walipe gharama" kwa waliyoyafanya enzi za ukoloni

Rais wa Ureno amesema, nchi yake inabeba dhima ya jiinai na uhalifu iliofanya wakati wa biashara ya utumwa kupitia Bahari ya Atlantiki na enzi ya ukoloni, na kupendekeza kuwaa kuna haja ya kufidia hali hiyo.

"Tunapaswa kulipa gharama," amesema Rais Marcelo Rebelo de Sousa na kuongeza kuwa Ureno inapaswa kutafuta njia za kurekebisha jinai ilizofanya. Mwaka jana, kiongozi huyo alisema nchi yake inapaswa kuchukua hatua kubwa zaidi kuliko kuomba msamaha tu. Ameyasema hayo katika hotuba ya kuadhimisha kumbukumbu ya kila mwaka ya Ureno ya Mapinduzi ya "Carnation" ya mwaka 1974, ambayo yaliupindua mfumo wa kidikteta wa nchi hiyo. Utawala mkubwa wa kikoloni wa Ureno ambao ulianzishwa katika karne ya 15 na kuwepo hadi karne ya 20, ulijumuisha pia kuyatawala mataifa kadhaa ya barani Afrika.

Mtandao huo wa ukoloni, hatimaye ulisamabaa kutoka Amerika hadi Japan.

 Jana Jumatano, vyombo vya habari vilimnukuu Waziri wa Brazil wa Usawa wa Rangi, Anielle Franco akieleza kwamba nchi yake imewasiliana na serikali ya Ureno kutangaza utayarifu wake wa kutoa msaada katika mchakato wa kuandaa hatua za ulipaji fidia. Halikadhalika, wiki iliyopita, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk alitilia nguvu wito wa mataifa ya Afrika na Caribbean wa kutaka madola ya kikoloni yachukue hatua ya kufidia hasara zilizoyasababishia mataifa hayo wakati wa enzi za utumwa na ukoloni.../

342/