Ayatullah Seyed Ahmad Khatami, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameashiria operesheni ya Ahadi ya Kweli ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuutia adabu utawala wa Kizayuni wa Israel na akabainisha kuwa: kisasi ulicholipiza Mfumo wa Kiislamu kwa utawala wa Kizayuni kilikuwa cha kumtia adabu mchokozi; na kama watataka kurudia kufanya upuuzi mwingine watachapwa kibao kikali zaidi.Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema, katika operesheni hiyo, adui alielewa vyema kwamba nara na kaulimbiu za Iran zinaandamana na vitendo na akaongeza kuwa: katika operesheni hiyo, vikosi vya ulinzi vya Iran vililenga vituo vilivyotumika kufanyia shambulio dhidi ya sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran tu mjini Damascus; na hatua hiyo imedhihirisha jinsi Iran inavyofanya mambo kwa busara na mantiki.
342/