Al-Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib(a.s) anasema :"Ninastaajabishwa na wale ambao hufikiria vyakula kwa ajili ya miili yao tu, lakini hawafikirii vyakula kwa ajili ya Roho zao. Wao huondoa vyakula vinavyowasumbua kutokea matumbo yao, na papo hapo wa wanazijaza nyoyo zao kwa mambo yanayoangamiza nyoyo zao." Safinatul Bihaar , juu ya kuonja
Maelezo mafupi :
Kama vile Al-Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. alivyosema, watu huwa wanajali mno vyakula vya kula, na hawali hadi wapo katika mwanga, na hawafungui vinywa vyao hadi pale macho yao yawapo wazi. Wao hujiepusha na vyakula vyote vyenye mashaka na wengi wao huzingatia maelfu ya hatua za afya na siha zao kwa ajili ya kuzilisha miili yao. Lakini, ama kuhusiana na vyakula vya Roho, wao, huku wakiwa wamefumba macho yao katika kiza kikali, wanajilisha vyakula vya nyoyo zao zenye kushukiwa, katika nyoyo zao. Wao kwa urahisi hukubalia maneno ya marafiki wasio wema, habari zisizo kweli na sahihi na usambazaji wenye sumu na mashaka, na kwa hakika haya ni yenye kushangaza mno.
Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho "MAFUNZO 150 KWA MAISHA BORA" - Ayatullah Makarim Shirazi