Aidha amesisitiza kuwa kundi lake limefufua uwezo wake wa kijeshi pia. "Tumethibitisha kupitia muqawama au mapambano kwamba hatutaruhusu adui (Mzayuni) kuendeleza ajenda yake. Ni jukumu la serikali ya Lebanon na jumuiya ya kimataifa kukabiliana na vitendo vya uchokozi vinavyoendelea (dhidi ya Lebanon).
Kiongozi wa Hezbollah alisema kuwa vuguvugu lake limepinga mipango ya upanuzi ya Israeli, akisisitiza kuwa sasa ni zamu ya serikali ya Beirut kujithibitisha kupitia hatua za kisiasa.
Sheikh Naim Qassem alitoa maoni hayo katika hotuba iliyorekodiwa kwenye Kongamano la Nne la Kimataifa la Kumuenzi Ayatullah Mohammad-Taqi Mesbah Yazdi, ambalo linafanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran, Jumatano.
Alisisitiza kuwa Hizbullah inastawi, na imeimarika, "Ina imani na watumishi waaminifu wanaoiwezesha kukua na kuwa na nguvu zaidi."
Kiongozi wa Hizbullah aliendelea kusema kuwa jeshi la Israel linaua kiumbe chochote kilicho hai katika Ukanda wa Gaza, likiangusha nyumba zote na kufanya mauaji ya kimbari katika eneo hilo la pwani lililozingirwa.
Sheikh Qassem alibainisha kuwa utawala wa Tel Aviv unatambulika kama utawala wa kinyama na wa jinai na ulimwengu wa Kiislamu na jumuiya ya kimataifa, akiongeza kuwa utawala huo unafanya ukatili huo kwa msaada wa Marekani ya jinai, ambayo yenyewe ni adui wa ubinadamu.
Chanzo: parstoday