KUTHIBITI KWA MWEZI WA RAMADHANI
Mas’ala: 1-Huzingatiwa katika kuthibiti kwa mwezi wa ramadhani na kuwajibika kufunga mwezi wa Ramadhani njia hizi zifuatazo:
1- Mukallaf auone mwezi yeye mwenyewe. 2- Apate yakini au matumaini kutokana na kuenea kwa habari za kuonekana kwa mwezi huo au habari zingine zithibitishazo suala hilo katika nchi yake au sehemu yenye hukumu kama hiyo.
3- Kupita siku thalathini za mwezi wa shaaban. 4-Kutoa ushahidi wanaume wawili waadilifu ya kuwa wameuona ( na hapo nyuma tumekwisha elezee maana ya uadilifu ) na huzingatiwa kuwa kinacho tolewa ushahidi kiwe ni kimoja, lau mmoja wao atadai ya kuwa ameuona mwezi katika upande fulani, na mwingine akadai ya kuwa ameuona upande mwingine, kwa ushahidi huo mwezi hautathibiti, kama ambavyo huzingatiwa kutokuwepo mpingaji wa ushahidi huo- hata kama kwa kuonyesha kitendo chenye hukumu kama hiyo ya kupinga- kama ikiwa kundi la watu fulani wa nchi hiyo watatoa habari za kuonekana mwezi na wakadai kuwa wameuona mwezi na miongoni mwao kukiwemo waadifu wawili, au wakatoa habari za kuonekana mwezi kundi fulani lakini hawakudai ya kuwa wameuona mwezi isipokuwa waadilifu wawili na wengine hawakuuona na miongoni mwao kukiwa na waadilifu wawili ambao ndio wanao wawakilisha katika kufahamu sehemu pekee iliyo onekana mwezi kwa kuangalia pamoja na anga kuwa safi na kutokuwepo kinacho tarajiwa kuwa ni kizuwizi cha kuuona mwezi, katika hali kama hii ushahidi wa watu wawili waadiofu hauna iitibari yoyote, isipo kuwa ikipatikana yakiini na matumaini kutokana na ushahidi wao.
Mas’ala: Mwezi hauthibiti kwa hukumu ya hakimu wala kwa kuwa kwake na duara iwe dalili ya kuwa ulikuwa ni wa usiku ulio pita, ndio ikiwa hukumu yake itampatia matumaini na kumthibitishia ya kuwa mwezu umeonekana katika nchi hiyo au sehemu ambayo hukumu yake ni sawa na nchi yake na hakutegemea kauli ya mtabiri au mnajimu au mfano wa hao.
Mas’ala: Ikiwa mukallaf atakula kisha ikabainika kuthibiti kwa hilali kupitia moja wapo kati ya njia zilizo tajwa itawajibika kuilipa funga hiyo, na ikiwa itathibiti huku imebakia sehemu ya mchana itawajibika kufunga sehemu hiyo iliyo bakia kutokana na kauli ya ahwat.
Mas’ala: Ina tosha kuthibiti mwezi katika nchi fulani hata kama si katika nchi ya mfungaji ikiwa machweo ya nchi hizo ni mamoja, kwa maana kuwa mwezi ukionekana katika nchi moja ni lazima uonekana katika nchi ya pili kama hakuna kizuwizi kama mawingu au mlima au mfano wa hayo, kwa hivyo ikiwa mwezi utaonekana katika nchi za mashariki ni lazima uwe umethibiti kwenye nchi za magharibi pia lakini kwa kuzingatia kuwa kusiwe na umbali zaidi katika machweo, ama ikiwa utathibiti katika nchi za magharibi si lazima kuthibiti katika mashariki isipokuwa ikiwa zinakaribiana katika machweo katika misitari ya(Al aradh)na hapakuwa na urefu wa kijografia wenye umbali wa kiasi cha kilometa (880).
Mas’ala: Ni lazima katika kuthibiti kwa mwezi wa shawwal kuthibiti mojawapo kati mambo yaliyo tangulia lau kamahalikuthibiti jambo lolote kati ya hayo haitajuzu kula.
Mas’ala: Ikiwa mtu atafunga siku yashaka katika mwezi wa shawwal, kisha mwezi ukathibiti katikati ya mchana itakuwa ni wajibu kwake kula.
Mas’ala: Haijuzu kufunga siku ya shaka ya mwezi wa ramadhani kwa kukusudia kuwa ni katika mwezi wa Ramadhani, ndio inajuzu kufunga kwa lengo kuwa ikiwa ni katika mwezi wa shaaban funga yake itakuwa ni funga ya sunna au kadhaa na ikiwa ni katika mwezi wa ramadhani itakuwa ni funga ya wajibu na funga yake itakuwa sahihi.
Mas’ala: Ikiwa itatokea kuwa mtu anaishi sehemu ambayo mchana wake ni miezi sita na usiku wake ni miezi sita au mchana wake ni miezi mitatu na usiku wake ni miezi tisa au mfano wa hivyo kauli ya ahwat ya wajibu ni kuwa ni juu yake kuangalia na kuchunga sehemu zilizo karibu nae ambazo zinapata usiku na mchana katika muda wa masaa ishirini na nne na atasali sala tano kulingana na wakati wa sehemu hizo kwa nia ya kujikurubisha kwa Allah moja kwa moja, ama katika funga itawajibika kwake kuhamia katika nchi ambayo anaweza kufunga, ima iwe ni katika mwezi wa ramadhani au baada ya ramadhan, na ikiwa hakuweza kufanya hivyo ni juu yake kutoa fidia, na ikiwa atakuwa katika nchi amabyo ina usiku na mchana katika muda wa masaa ishirini na nne- hata kama mchana wake ni masaa ishirini na tatu na usiku wake ni saa moja au kinyume chake- sala yake itasaliwa kulingana na wakati wake maalum katika nchi hiyo, ama funga ya mwezi wa ramadhan ni wajibu kwake kuitekeleza katika wakati wake hata kama utapungua, maadam jua lina chomoza na kuzama na ita anguka ikiwa hakuweza na ikiwa ataweza kuilipa ni wajibu kuilipa la sivyo ni juu yake kutoa fidia.
NIA YA FUNGA (SWAUMU)
Ni wajibu kwa kila mukallaf kukusudia kujizuwia na mambo yanayo funguza ambayo yanajulikana, kuanzia alfajiri inapo chomoza hadi linapo zama jua kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah mtukufu, na kauli ya adh’har ni kuwa inajuzu kutosheka na makusudio ya kufunga mwezi mzima toka mwanzo wake, kwa hiyo haizingatiwi kukusudia katika kila usiku au kutia nia kila siku au wakati wa kuchomoza alfajiri japo kuwa huzingatiwa kuwepo kwa nia hiyo hata kama ni kwa kujua kuwa ni kitu gani akifanyacho.
Mas’ala: Kama ambavyo huzingatiwa nia katika mwezi wa ramadhani vile vile huzingatiwa katika funga zingine za wajibu, kama funga ya kafara, nadhiri , kadhaa, na funga kwa niaba ya mtu mwingine, lau kama mukallaf atakuwa na jukumu la kutekeleza funga kadhaa za wajibu ni juu yake kuziainisha kwa kuongezea katika makusudio yake (Nia), ndio hakuna haja ya kuainisha katika mwezi wa ramadhani kwa sababu funga katika mwezi wa ramadhani inajitambulisha yanyawe.
Mas’ala: Katika nia ya funga inatosha kunuwia kuwa ninajizuwia na vitu ninavyo funguza kwa sura ya ujumla na hakuna haja ya kuviainisha kila kimoja.
Mas’ala: Ikiwa mtu hakutia nia siku moja wapo katika mwezi wa ramadhani kwa kusahau ya kuwa yuko ndani ya mwezi wa ramadhani kwa mfano na hakula kitu chochote, ikiwa atakumbuka baada ya kupinduka kwa jua ni wajibu wake kutokana na kauli ya ahwat ya wajibu kufunga sehemu ya chana iliyo bakia kwa makusudio ya kujikaribisha kwa Allah na baadae atailipa,na ikiwa atakumbuka kabla ya kupinduka kwa jua atanuwia funga na funga hiyo itatosheleza kutokana na kauli ya adh’har japo kuwa kauli ya ahwat inasema kuwa inabidi kuilipa baada ya hapo, vile vile katika funga zingine za wajibu ambazo ni maalum, ama funga za wajibu ambazo si zenye kuainishwa wakati na nia yake huendelea hadi jua linapo pinduka, ama funga ya sunna wakati wake wa kutia nia hurefuka hadi kufikia magharibi kwa maana kuwa mukallaf ikiwa hakula inajuzu kwake kutia nia ya sunna na kufunga sehemu ya mchana iliyo bakia hata kama itakuwa imebakia sehemu ndogo ya mchana na huhesabiwa kuwa amefunga siku hiyo.
Mas’ala: Lau kama mtu atanuwia funga kisha akanuwia kula au akakusudia kula katika wakati ambao haijuzu katika wakati huo kuchelewesha nia kwa makusudi kisha akabadilisha tena nia kwa kauli ya ahwat nia hiyo haitatosheleza.
Mas’ala: Ikiwa mukallaf atakusudia usiku kufunga siku ya kesho, kisha akalala na hakuweza kuamka mchana kutwa funga yake ni sahihi, ama ikiwa atalala hadi kupinduka kwa jua na hakutia nia kabla, kauli ya ahwat ni kuwa atatimiza siku ile kisha atailipa kadhaa.