Main Title

source :
Jumamosi

19 Machi 2011

20:30:00
256950

YANAYO FUNGUZA SWAUMU

YANAYO FUNGUZA SWAUMU

Mambo yafunguzayo swaumu ni haya yafuatayo: 1-2 (Kukusudia kula na kunywa)

Na hakuna tofauti katika vitu viliwavyo na vinywewavyo sawa viwe ni vile vijulikanavyo au vinginevyo, wala hakuna tofauti kati ya chakula hicho kiwe kingi au kichache, kama ambavyo hakuna tofauti katika kula na kunywa iwe ni kwa njia ya kawaida au njia nyingineyo, lau kama mtu atakunywa maji kwa kupitia puani funga yake inabatilika, na funga itabatilika kwa kumeza chembe chembe za chakula zilizo bakia katika kinywa au kwenye meno kwa hiyari.

Mas’ala: Funga haibatiliki kwa kula au kunywa kusiko kwa makusudi, kama akisahau na akala au kunywa, vile vile haibatiliki ikiwa atavitapitiliza kwenye koo lake bila hiyari au mfano wa hayo.

Mas’ala: Haibatiliki funga kwa kujiwekea dawa kupitia njia ya sindano katika viungo fulani au kwenye mishipa, hata kama itakuwa inafanya kazi ya chakula kama vyakula vilivyo zoweleka katika zama zetu kama ambavyo haibatiliki kwa kudondoshea matone masikioni au machoni hata kama itadhihiri athari zake kama rangi au ladha kooni.

Mas’ala: Ina juzu kwa mwenye funga kumeza mate kwa hiyari yake ikiwa bado hayajatoka mdomoni mwake bali inajuzu kwake kuyakusanya mdomoni kisha kuyameza.

Mas’ala: Hakuna shaka kwa mwenye kufunga kumeza makoozi yatokayokifuani au yatokayo kichwani ikiwa hayaja fika mdomoni ama yakifika mdomoni kauli ya ahwat ni kuto yameza.

Mas’ala: Ina juzu kwa mwenye kufunga kupiga mswaki, lakini ikiwa mswaki utatoka mdomoni haijuzu kuurudisha mdomoni hali ya kuwa una umajimaji isipokuwa ikiwa atayatema mate yaliyomo mdomoni mwake baada ya kuurudisha, ndio ikiwa maji maji yatakuwa machache kuliko mate yaliyomo kinywani mwake kiasi kwamba maji maji yale hayakuonekana yaliyo toka nje, hapo inajuzu kuyameza.

Mas’ala: Ina juzu kwa mwenye kutaka kufunga kuacha kuchokonoa meno baadaya kula ikiwa atafahamu ya kuwa hakuna vyakula vilivyo ingia na kubakia kwenye meno hadi katikati ya mchana, laa sivyo itakuwa ni wajibu kuchokonoa meno hayo.

Mas’ala; Hakuna shaka kwa mwenye funga kumtafunia mtoto chakula au mnyama na inajuzu kuonja mchuzi na mfano wa hayo kati ya vitu ambavyo havi vuki na kufika kooni, lau kama itatokea chembe za chakula kuvuka na kufika kooni bila ya kukusudia wala kujua ya kuwa itavuka kwa nguvu au kwa kusahau funga yake haitabatilika.

Mas’ala; Inajuzu kwa mwenye kufunga kusukutua maji kinywani kwa malengo ya kutawadha au kwa ajili ya malengo mengine kwa sharti kuwa asimeze chembe yoyote ya maji kwa makusudi, na ni sunna baada ya kusukutua ateme mate mara tatu.

Mas’ala: Ikiwa mwenye kufunga ataingiza maji kinywani mwake kwa ajili ya kusukutua au kwa sababu nyingine na maji yakapitiliza hadi kooni mwake bila hiyari yake ikiwa aliyaweka akiwa na kiu kwa ajili ya kupoza koo au kinywa ni wajibu kwake kuilipa, ama ikiwa alifanya hivyo tofauti na hivyo kati ya sehemu zinazo bidi kuingiza maji kinywani au puani na kuvuka hadi kooni bila ya hiyari yake kauli ya adh’har ni kuwa si wajibu kulipa japo kuwa kauli ya ahwati ni kuwa hata lipa ikiwa alifanya hivyo katika hali ya kutawadha kwa ajili ya sala ya sunna bali kwa kitendo chochote ikiwa haikuwa ni kwa ajili ya sala ya sunna bali hata kama haikuwa ni kwa ajili ya sala ya faradhi.

Mas’ala: (Kitu cha tatu kati ya vitu vinavyo funguza: kutokana na kauli ahwat ni kuzowea kumsingizia mwenyezi mungu na mtume wake uongo au yeyote kati ya maimam watakasifu juu yao amani) na huunganishwa na fatimas asswiddika alie twaharika na mitume wengine na mawasii wao amani iwe juu yao.

Mas’ala: Ikiwa mwenye kufunga ataitakidi ya kuwa habari alizo zitoa kuhusiana na mwwenyezi mungu au mmoja wapo kati ya maasumiina ya kuwa ni za kweli kisha ikambainikia kuwa ni uongo funga yake haita batilika, ndio ikiwa atatoa habari kuhusiana na mwenyezi mungu au kuhusu mtume wake bila kujitegemeza kwenye hojja ya kisheria pamoja na kuwa kulikuwa na ihtimali ya kuwa habari hizo ni uongo na kweli habari hizo zikawa ni uiongo hukumu yake ni sawa na hukumu ya kukusudia kusema uongo.

Hakuna shaka kuwa inafaa kusoma qur ani kwa kukosea ikiwa msomaji hakuwa katika hali ya kutoa masimulizi yaliyo teremshwa katika qur ani, na funga yake haitabatilika kwa kufanya hivyo.

Mas’ala: Jambo la nne kati ya vitu ninavyo funguza: - kwa kauli iliyo mashuhuri- (kupiga mbizi kwenye maji kwa makusudi) lakini kwa kauli iliyo adh’har ni kuwa haidhuru katika kuswihi kwa funga bali ni makruhu karaha iliyo kubwa, na hakuna tofauti katika swala hilo kati ya kuzamisha kiwili wili chote au kichwa pekee, na hakuna shaka yoyote kwa mwenye kufunga kusimama chini ya mvua huku ikinyesha na mfano wa hilo hata kama maji yataufunika mwili wake wote.

Mas’ala: Kuli ya ahwat inasema kuwa ni juu ya mwenye kufunga katika mwezi wa ramadhani na katika funga zingine kuto piga mbizi au kuzamisha kicha katika maji japo kuwa kauli ya adh’har inasema kuwa inajuzu kufanya hivyo.

Mas’ala: Jambo latano kati ya vitu vinavyo funguza:( Kukusudia kufanya tendo la kijinsia ambalo hupelekea kupata janaba) na funga haitabatilika kwa kufanya tendo hilo ikiwa si kwa makusudi.

Mas’ala: Jambo la sita kati ya vitu vinavyo funguza:( kupiga kunyeto kwa kuchezea kiungo cha kiume au kuibusu (kuinyonya) au kuichezea kwa kuigusa na mengineyo yasiyo hayo) bali akifanya chochote kati ya hayo, na alifanya hivyo bila kuwa na uhakika ya kuwa manii hayatatoka, kwa ghafla yakatoka funga yake itabatilika kutokana na kauli ya adh’har.

Mas’ala: Ikiwa mtu atajiotea katika mwezi wa ramadhani inajuzukwake kufanya istibraa kwa kukojoa na awe na yakini ya kuwa chembe chembe zilizo bakia za manii zimetoka katika mirija ipitayo manii bila ya kutofautisha ya kuwa istibra hiyo iwe kabla ya kuoga au baada ya kuoga japo kuwa kauli ya ahwat inasema kuwa ni bora kuacha katika sehemu ya pili (yaani baada ya kuoga).

Mas’ala: Jambo la saba kati vitu vinavyo funguza :( Kukusudia kubakia na janaba hadi kuchomoza kwa alfajiri) na hukumu hii inahusika tu na funga ya mwezi wa ramadhani na kadhaa yake, ama katika funga zingine kati ya mgawanyiko wa funga kauli ya dhahiri ni kuwa funga haita batilika katika hali kama hiyo japo kuwa kauli ya ahwat ni kuwa ni bora kuiacha katika funga zingine za wajibu, kama ambavyo kauli ya ahwatul awlaa ni kuto ilipa funga ya mweziwa ramadhani katika siku ambazo atabakia akiwa na janaba hadi kuchomoza kwa alfajiri bila ya kukusudia.

Mas’ala: Kubakia na hadathi ya hedhi au Nifasi pamoja na kuwepo uwezekano wa kuoga au kutayammam hukumu yake ni sawa na tuliyo seme kwa mwenye kukusudia kubakia kwernye janaba bali hata kwa mwenye kulipa kadhaa pia kutokana na kauli ya ahwat tofauti na funga zungine.

Mas’ala: Mwenye kupatwa na janaba katika usiku wa mwezi wa ramadhani, kisha akalala bila ya kukusudia kuoga- ikiwa alinuwia kuto oga, bali vile vile ikiwa atakuwa ni mwenye wasi wasi kuhusiana na ghusli hiyo- na akaamka baada ya alfajiri hukumu yake ni sawa na hukumu ya alie kusudia kubakia kwenye janaba, ama ikiwa alikusudia kuoga janaba na akawa na yakini ya kuwa ataamka- kutokana na kuzowea au jambo lingine- ikatokea kuwa hakuweza kuamka isipokuwa baada ya alfajiri hakuna jukumu lolote juu yake na funga yake ni sahahi, ndio ikiwa ataamka kisha akalala na hakuweza kuamka hadi ikachomoza alfajiri ni wajibu wake kulipa kadhaa baada ya kumalizika, vilevile hali ni hiyo hiyo ikiwa atalala mara tatu isipo kuwa ni kwamba kutokana na kauli ya ahwatul awlaa ni kuwa atatoa kafara katika siku hiyo pia.

Mas’ala: Ikiwa atapatwa na janaba katika usiku wa mwezi wa ramadhani na akalala hali ya kuwa amenuwia au amekusudia kuoga lakini hakuwa na yakini ya kuwa ataweza kuamka, kauli ya ahwat ni kuwa ni lazima kuoga kabla ya kulala, na ikiwa atalala na hakuweza kuamka kauli ya ahwat ni kuwa atailipa funga hiyo hata katika ulalaji wake wa mwanzo, bali kauli ya ahwat ni kuwa atatoa kafara pia na hasa katika ulalaji wake wa tatu.

Mas’ala: Ikiwa mukallafu ataelewa ya kuwa anayo janaba lakini akasahau kuoga janaba hiyo hadi kuchomoza kwa alfajiri ya mchana wa mwezi wa ramadhani itakuwa ni juu yake kuilipa funga hiyo lakini ni wajibu wake kufunga siku hiyo kwa makusudia ya kutekeleza wajibu ulioko kwenye dhima yake kutokana na kauli ya ahwat, na kauli yenye nguvu zaidi ni kuwa hukumu hii haitaunganishwa na funga isiyo kuwa ya mwezi wa ramadhani katika suala hilo hata katika kadhaa yake kama ilivyo tangulia, na kikiwa hakufahamu ya kuwa alikuwa na janaba au ali fahamu ya kuwa ana janaba na akasahau wajibu wa kufunga siku ya kesho hadi ikachomoza alfajiri funga yake itakuwa sahihi na hakuna lolote juu yake.

Mas’ala: Ikiwa mwenye janaba hakuweza kuoga usiku, ni wajibu wake kutayammam kabla ya kuchomoza alfajiri badala ya kuoga na ikiwa ataacha kutayammam funga yake itabatilika kutokana na kauli ya adh’har, na si wajibu kwake kubakia akiwa macho baada yake hadi kuchomoza kwa alfajiri japo kuwa kufanya hivyo ni ahwat, na ikiwa alikuwa na uwezo wa kuoga na hakufanya hivyo hadi muda ukawa finyu na hakutayammam, funga yake itabatilika.

Mas’ala: Hukumu ya mwanamke katika hali ya istihadha ndogo ni sawa na hukumu ya mwenye twahara, ama katika istihadha nyingi kauli iliyo mashuhuri ni kuwa huzingatiwa kuoga ghusli za mchana na usiku ulio pita katika kuswihi kwa funga yake, lakini kauli ya kuto zingatia uogaji huo haiko mabali japo kuwa kufanya hivyo ni ahwat, bali kauli ya ahwati ni kuwa inambidi kuoga kwa ajili ya salaya asubuhi kabla ya kuchomoza alfajiri kisha atarudia baada yake, ama katika hali ya istihadha mutawassit kauli iliyo adh’har ni kuwa hataizingatia ghusli hiyo katika kusihi kwa funga yake, japo kuwa kauli ya ahwat ni kuwa itambidi kuoga pia.

Mas’ala: jambo la nane kati ya vitu ninavyo funguza: (Kukusudia kuingiza vumbi au moshi mzito kooni kwa kauli ya ahwat) na hakuna shaka ikiwa vumbi hilo au moshi huo si mzito, vile vile moshi au vumbi ambalo ni vigumu kujikinga nalo kwa kawaida kama vumbi lililo timuliwa na hewa au upepo.

Mas’ala: jambo la tisa kati ya vitu vinavyo funguza:( Kujitapisha kwa makusudi) na inajuzu kwa mwenye kufunga kupiga mbwewe hata kama atakuwa na ihtimali ya kutoka kwa chembe za chakula au kinywaji kwa pamoja na kauli ya ahwat ni kuwa ni bora kuto fanya hivyo ikiwa atakuwa na yakini ya kutoka kwa chakula.

Mas’ala: Ikiwa atapiga mbori na kutoka chakula hadi kooni au kikatoka kwa sababu nyingine ile bila ya kukusudia haita juzu kukimeza kwa mara ya pili, na ikiwa atakimeza hukumu yake ni sawa na hukumu ya kula na kunywa kwa kauli ya ahwat.

Mas’ala: Jambo la kumi kati ya vitu vinavyo funguza:( Kukusudia kuingiza maji mwilini kupitia mishipa au njia nyingioneyo au chochote chenye maji maji) hakuna shaka ikiwa kitu hicho hakina umaji maji.

Mas’ala: Nyongeza: - Mambo yafunguzayo yaliyo tangulia- tofauti na kula na kunywa na kufanya tendo la kijinsia- hubatilisha funga ikiwa yatafanywa na mwenye kufahamu ya kuwa ni vitu vinavyo funguza au jahili mukaswir ( yaani asie fahamu na kuto fahamu huko hakutokani na uzembe wake), vile vile asie kuwa mukassir ikiwa alikuwa ni mwenye kutaradadi, na hilo haliifanyi funga kubatilika ikiwa atafanya bila kukusudia katika kuto kufunguza kwake kwa hoja ya kisheria au kutokana na ujahili murakkab ikiwa imetokana na uzembe wake mwenyewe.

HUKUMU YA VITU VINAVYO FUNGUZA

Ni wajibu kutoa kafara kwa kila mwenye kuacha kufunga mwezi wa ramadhani kwa kula au kunywa au kufanya tendo la kijinsia au kupiga kunyeto au kubakia na janaba kwa makusudi na kwa hiyari bila ya kulazimishwa wala kukarahishwa, na inathibiti kafara kwa kumkomboa mtumwa au kuwalisha masiki sitini au kufunga miezi miwili mfululizo, yaani kufunga mwezi wa kwanza kamili na katika mwezi wa pili akafunga japo kuwa siku moja, na siku zilizo bakia akazifunga siku yoyote ile, na hii ikiwa futari aliyo itumia ni ya halali ama ikiwa ni ya haram, kauli ya ahwatul awlaa ni kuwa atatekeleza mambo yote yaliyo tajwa na kama hakuweza kuyatekeleza yote atatekeleza tu yale awezayo kuyatekeleza.

Mas’ala: Ikiwa mwenye kufunga atamlazimisha mkewe kufanya tendo la ndoa katika mchana wa mwezi wa ramadhani nae akiwa amefunga kafara zitaongezeka juu yake kutokana na kauli ya ahwat na ata adhirishwa hadharani kutokana na hukumu ya hakimu wa kisheria, na ikiwa hakumlazimisha na akafanya kitendo hicho kwa ridhaa yake mwamamke ni juu ya kila mmoja kutoa kafara moja na wata adhiriwa kulingana na aonavyo hakimu wa kisheria pia.

Mas’ala: Mtu yeyote atakae kula katika siku ya funga ya mwezi wa ramadhani na funga yake kubatilika ni wajibu kwake kujizuwia kula sehemu iliyo bakia ya siku hiyo moja kwa moja kwa kauli ya ahwat, bali kauli ya ahwat ni kuwa kujizuwia huko kuwe ni kwa makusudio ya kujikaribisha kwa Allah katika kuingiza moshi au vumbi zito kooni na katika kumzulia mwenyezi mungu na mtume, na kafara haiwi wajibu isipo kuwa kwa ulaji wa mara ya kwanza na haikaririki kwa kula mara kadhaa hata katika kufanya tendo la kijinsia na kupiga kunyeto hakika kauli ya adh’har ni kuwa kafara haikaririki kwa kukaririka kitendo hicho japo kuwa ni ahwat kufanya hivyo.

Mas’ala: Mwenye kula katika mwezi waramadhani kwa makusudi kisha akasafiri, wajibu wa kutoa kafara hauta anguka hata kama safari yake itakuwa kabla ya kupinduka kwa jua.

Mas’ala: Wajibu wa kutoa kafara unahusika na mwenye kufahamu hukumu, hakuna kafara kwa mtu asie fahamu hukumu, kutofahamu huko kutokane na uzembe wake au laa- na asiwe mwenye kutaradudi-kwa kauli ya adh’har, lau kama atatumia kitu kinacho funguza kwa kuitakidi ya kuwa hakibatilishi funga haita kuwa ni wajibu kwake kutoa kafara sawa awe ameitakidi kuwa ni haramu katika nafsi yake au laa kwa kauli iliyo aqwaa, lau kama atapiga kunyeto kwa makusudi akifahamu uharamu wa kufanya hivyo akiitakidi- hata kama ni kwa uzembe wake mwenyewe- kuto batilika kwa funga kwa kufanya hivyo hana jukumu la kutoa kafara, ndio haizingatiwi katika wajibu wa kutoa kafara kufahamu kuwa ni wajibu na haijuzu kujionyesha kuwa hukufunga katika mwezi wa ramadhani ikiwa kufanya hivyo itahesabiwa kuwa ni kuvunja na kuto uheshimu mwezi wa ramadhani isipo kuwa kwa mwenye udhuru, na ambae udhuru wake huonekana katika mandhari yake kama mtu kikongwe au mgonjwa ambae zinaonekana kwake dalili za ugonjwa na kauli ya ahwat ya wajibu ni kuwa ni bora kutompatia chakula mwenye matatizo kwa makusudi na sio kwa udhuri.

SEHEMU AMBAZONI WAJIBU KULIPA TU

Mas’ala:Mwenye kula katika mwezi wa ramadhani kutokana na udhuru au ugonjwa na mfano wa hayo ni wajibu wake kulipa siku hiyo katika miezi mingineyo na katika siku zingine za mwaka huo isipo kuwa siku mbili za idi (iidul fitri na idul adh’haa) haijuzu kufunga kadhaa katika siku mbili hizi au funga nyingine yoyote isiyo ya kadhaa kati ya funga zingine kama funga za sunna.

Mas’ala: Mwenye kulazimishwa kula au kunywa au kufanya tendoa la kijinsia katika mwezi wa ramadhani au kutokana na takiyya ikamlazimu kufanya tendo hilo au alilazimika kufanya hivyo au alilazimika kutapika au kujichoma dawa, inajuzu kwake kula kwa kiwango au kisi cha dharura ilivyo, lakini funga yake inabatilika na niwajibu kwake kuilipa bali kauli ya ahwat ni kuwa ni lazima kuilipa ikiwa atalazimishwa kula tofauti na sehemu tatu zilizo tangulia vilevile.

Mas’ala: Katika sehemu zilizo tangulia zimetajwa sehemu zinazowajibika kulipa tu na zingine ni kamazifuatazo:

1- Pindi nia ikiingiwa na kasoro katika mwezi wa ramadhani lakinihakufanya jambo lolote linalo funguza kati ya mambo yaliyo tajwa.

2- Pindiakifanya jambo moja wapo kati ya mambo yafunguzayo bila ya kufanya uchunguzi kama alfajiri imechomoza, na wakati anakula ikadhihiri ya kuwa alfajiri imekwisha chomoza, wakati huo ni wajibu wake kutokula kwa malengo ya kujik