Main Title

source : Radio Tehran
Jumamosi

19 Machi 2011

20:30:00
265106

Makala maalumu

Tukio la 9/11, kisingizio cha vita dhidi ya Uislamu

Leo ikiwa ni kumbukumbu ya matukio ya September 11, nchini Marekani, wataalamu wa masuala ya kisiasa wanasema Marekani inatumia matukio hayo kuendeleza vita na chuki dhidi ya Uislamu duniani.

Ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA-bukumbu ya matukio ya September 11, nchini Marekani, wataalamu wa masuala ya kisiasa wanasema Marekani inatumia matukio hayo kuendeleza vita na chuki dhidi ya Uislamu duniani.

Saeb Shaath, mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati, katika maohojiano na Press TV amesema, baada ya hujuma za Septemba 11 mwaka 2001, serikali ya Marekani imekuwa ikitumia vyombo vya habari kueneza propaganda kuwa usalama umekosekana Marekani kutokana na Waislamu wanaoishi nchini humo. Aidha Marekani pia inatumia vyombo vya habari vya Kimagharibi kueneza chuki dhidi ya Uislamu kote duniani.

Saeb Shaath ameongeza kuwa chuki dhidi ya Uislamu imeambatana na hujuma ya kijeshi ya Marekani dhidi ya nchi za Kiislamu kama vile Afghanistan na Iraq kwa kisingizio cha kupambana na kile kinachotajwa ni ugaidi. Ametoa mfano wa hujuma ya kijeshi ya Marekani huko Iraq ambayo imepelekea watu karibu milioni 2 kuuawa na wengine milioni tano kufanywa wakimbizi.

Viongozi wa Marekani wametangaza kuwa wamepokea vitisho ambavyo havijathibitishwa kuhusu uwezekano wa kufanyika mashambulio ya kigaidi katika shughuli ya kukumbuka matukio ya Septemba 11.

Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, suala la ugaidi na mashambulio dhidi ya maslahi ya Marekani ndani na nje ya nchi hiyo vimekuwa changamoto kwa wanasiasa, duru za habari na wananchi wa Marekani. Marekani ni nchi ambayo kwa hali zote na wakati wowote inaweza kukabiliwa na machafuko, vitendo vya ugaidi na mauaji. Serikali ya Marekani inawaruhusu raia kubeba silaha na kuna silaha milioni 200 za aina mbalimbali kati ya jamii ya watu milioni 300 wa nchi hiyo. Huko Marekani pia ghasia na utumiaji mabavu vimekita mizizi katika jamii kuliko nchi yoyote ile nyingine duniani. Hii ni katika hali ambayo, makundi mengi ya wanamgambo wanaobeba silaha yanaendesha harakati zao nchini humo na baadhi ya makundi hayo yanaonekana kutoa kipaumbele utumiaji wa silaha na mabavu katika shughuli zao.

Wakati huo huo uingiliaji kati, kupenda kujitanua na kuendesha vita kunakofanywa na viongozi wa Marekani katika uga wa kimataifa, kumeipelekea nchi hiyo kuwa mlengwa halisi wa mashambulio ya makundi yanayopinga siasa za kijuba za Marekani. Kuhusiana na suala hilo, inaonekana kuwa baadhi ya wanastratejia wa Marekani wanahitaji kutumia kisingizio cha kuweko vitisho vya ugaidi ili kufanikisha siasa za nje za Washington na iwapo vitisho kama hivyo havitakuwepo basi zinatanyika jitihada za kuzusha vitisho bandia. Kwa maana nyingine ni kuwa, siasa za nje na za kiusalama za Marekani zitakabiliwa na matatizo bila ya kuwepo vitisho.

Katka miaka iliyopita suala la kupambana na hatari ya ukomonisti lilikuwa chachu kwa siasa za ndani na nje za serikali za Marekani na baadaye ilifuatia zamu ya Uislamu iti wenye misimamo mikali kama unavoitwa na Marekani na hatimaye vita dhidi ya ugaidi. Ngoma hizo za vitisho vya kigaidi na nara za kupambana nao zinakidhi baadhi ya mahitaji ya kisiasa, kiusalama na hata kiuchumi ya Marekani. Miongoni mwa malengo ya kueneza hufu, kubuni adui bandia na vitisho eti vya kigaidi ni pamoja na kutaka kufunika matatizo ya ndani ya Marekani, kuhalalisha vita vya nchi hiyo katika nchi za kigeni, kuhalalisha na kutetea matumizi ya mabilioni ya dola katika masuala ya kijeshi, kupeleka majeshi ya Marekani katika pembe mbalimbali dunia na kadhalila