Main Title

source :
Jumamosi

19 Machi 2011

20:30:00
270799

Falsafa ya Kiislam

Falsafa

Neno fasalfa si neno geni, kwani tumekuwa tukilisikia au kilitumia mara kwa mara katika mazungumzo yetu ya kila siku. Katika mada hii nitaelezea elimu ya Falsafa muhtasari. Neno Falsafa, linatokana na neno la kigiriki PHILOSOPHIA. Ambapo ni muunganiko wa maneno mawawili: PHILO na SOPHIA. Neno PHILO linamaanisha Upendo na neno SOPHIA lina maansiha hekima.

Neno fasalfa si neno geni, kwani tumekuwa tukilisikia au kilitumia mara kwa mara katika mazungumzo yetu ya kila siku. Katika mada hii nitaelezea elimu ya Falsafa muhtasari.    Neno Falsafa, linatokana na neno la kigiriki PHILOSOPHIA. Ambapo ni muunganiko wa maneno mawawili: PHILO na SOPHIA.Neno PHILO linamaanisha Upendo na neno SOPHIA lina maansiha hekima.       Hivyo basi neno PHILOSOPHIA au FALSAFA linamaanisha upendo wa hekima.Kwa kuzingatia maana ya neno Falsafa, tunakuta kuwa neno hili lina maana tofauti kabisa na ile ambayo sisi huitumia katika mazungumzo yetu ya kila siku.     Katika mazungumzo yetu ya kila siku neno Falsafa hutumika kuelezea itikadi, imani au mwenendo wa mtu au kundi fulani.Mfano: Falsafa ya maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w) au falsafa ya chama fulani.        Katika mada hii ninazungumzia Falsafa kwa maana ya Upendo wa hekima nasio ile maana iliyozoeleka katika mazungumzo yetu ya kila siku.    Historia ya neno Falsafa: wataalamu katika kuelezea histori ya neno falsafa wamegawanyika katika makundi matatu:1.Kundi la kwanza linasema kuwa mtu wa kwanza kutumia neno falsafa alikuwa ni Fithagoras (Pythagoras) ambaye aliishi karne ya sita kabla ya kuzaliwa kristo. Fithagoras anaitikadia kuwa Hekima ni katika sifa mahsusi za Mwenyezi Mungu nahii ndio sababu ya yeye kujiita Philosopher (mpenda hekima).2.Kundi la pili linasema kuwa mtu wa kwanza kutumia neno hili alikuwa ni Haruduut ambapo alilitumia neno hili katika Tarekhe yake karne ya tano kabla ya kristo.3.Kundi la tatu linasema kuwa mtu wa kwanza kutumia neno hili alikuwa ni Sokrate ambapo alilitumia neno hili akiwa dhidi ya kikundi cha Sophist ambao waliitumia hoja potofu kubadilisha ukweli wa mambo.Huu ni muhatasari maana na matumizi ya neno falsafa,katika mada itakayofuata tutachambua neno falsafa katika istilahi za kielimu.