Katika mada iliyopita niliahidi kuelezea baadhi ya makundi uislamu na itikadi zao na sasa umefika muda wa mimi kutekeleza ahadi yangu. Kuwapo makundi, tofauti na madhehebu kwa waislamu ni jambo lisilopingika, ila jambo la kuzingatia ni kwamba tofauti hizo si kubwa kiasi cha kuvunja umoja wa waislamu. Tukirudisha tarehe nyuma mpaka zama za Mtume wetu mtukufu Muhammad (s.a.w) tutakuta kwamba katika kipindi cha uhai wa mtume (s.a.w) waislamu walikuwa ni kitu kimoja na hakukuwa na kundi hata moja, kwani lilipo watatiza jambo moja kwa moja walikwenda kuuliza mtume(s.aw) naye aliwajibu.hivyo basi hakukuwa na tofauti za mitazamo wala rai kipindi cha uhai wa mtukufu Mtume (s.a.w). Baada ya mtume wetu Muhammad (s.a.w) kuondoka katika dunia hii tofauti zilianza na zikakithiri hata kutokea makundi na madhehebu mengi kama ilivyo sasa.ingawa makundi ni mengi katika uislamu ila makundi yote hayakutofautiana katika itikadi za misingi ya dini bali yote yaamini kumba: Mwenyezi Mungu ni mmoja,nakuwa Muhammad (s.aw) ni mtume wake.wote wanaamini Qur ani,ufufuo pia ya siku ya malipo.Pia hawakutofautiana katika mambo ya dharura katika uislamu kama vile Wajibu wa kusali, kutoa zaka, kuhiji na kufunga. Hivyo tofauti kubwa ya waislamu ilikuwa ni katika mitazo ya kiitikadi na kifiqh kama tulivyo eleza katika mada iliyopita.BAADHI YA TOFAUTI Tofauti katika masuala ya kifiqhi ndio sababu kuu ya kupatikana makundi ya kifqh kama vile madhehebu makuu manne ya kifqh kwa masunni ambayo ni Hanafii, Malikii, Shafii na Hanbalii makundi haya manne katika mtazamo wa kifqh yanatofautiana kwani kila moja kati ya makundi hayo yana rai yake binafsi ijapokuwa kuna wakati wanafikiana katika rai zao. Moja ya tofauti zao ni: suala la kumgusa mwanamke je? kunatengua udhu au lah:Shafii :( katika kitabu chake Al-umm Juzuu 1 kurasa 15) asema: kumgusa mwanamke kunatengua udhu.Hanafii :( katika kitabu chake cha Badaaius-sanaiu juzuu 1 kurasa 30) asema: kumgusa mwanamke hakutengui udhu.Maalikii :( katika kitabu chake Al-mudawwanatul kubraa juzuu 1 ukurasa 13) asema. Ikiwa atamgusa mwanamke kwa matamanio au makusudi basi kunatengua udhu nasi kinyume na hivyo.Ila makundi hayo yote ya masunni yanachukua mitazamo ya misingi ya dini kwa kundi la Ashaaira. ama tofauti kubwa iliyosababisha umma wa kiislamu kugawanyika ni suala la (ukhalifa) uongozi wa umma baada ya Mtume Muhammad (s.a.w).Tofauti hii iliwafanya waislamu kugawanyika katika makundi makuu mawili:Kundi la kwanza: lilisema kuwa mtume (s.a.w) kabla ya kifo chake aliainisha na kuteua atakaye kuwa Khalifa baada yake.ambapo walisema mteule huyo ni Amirul muuniin Ali bin Abii Taliib.Kundi la pili: lilisema kuwa mtume (s.a.w) hakuainisha wala kuteua atakaye kuwa Khalifa baada yake bali aliwaachia waislamu wamchague khalifa wampendao, hivyo wakamchagua Abubakar kuwa Khalifa. Kundi la kwanza kwa sasa ni maarufu kwa jina la Ahlul Bayt au Mashia.na kundila pili ni maarufu kwa jina la Ahlu Sunna au masunni. Haya ndio makundi makuu katika uislamu na makundi mengine yanaweza kuwa ni matawi ya makundi haya.tofauti kati ya makundi haya si kubwa kiasi cha kukafirishana, ijapokuwa kwa sasa siasa potofu zimeingizwa katika uislamu hata kufikia kundi moja kulikafirisha kundi lingine.Allah akitupa taufiki nitajitahidi kulielezea Kundi la kwanza kwa muhtasari
source :
Jumamosi
19 Machi 2011
20:30:00
278104
AKIDA Tofauti katika masuala ya kifiqhi ndio sababu kuu ya kupatikana makundi ya kifqh kama vile madhehebu makuu manne ya kifqh kwa masunni ambayo ni Hanafii, Malikii, Shafii na Hanbalii makundi haya manne katika mtazamo wa kifqh yanatofautiana kwani kila moja kati ya makundi hayo yana rai yake binafsi ijapokuwa kuna wakati wanafikiana katika rai zao.