Main Title

source :
Jumamosi

19 Machi 2011

20:30:00
295394

Akida sehemu ya Tatu Na:Sirkatundu

MAKUNDI KATIKA UISLAMU

Katika mada iliyopita nilielezea kuwa Ukhalifa au ungozi baada ya mtume saw ilikuwa ni sababu iliyopelekea waislamu kugawanyika makundi mawili Shia na Sunni

Ambapo masuni walidai kuwa mtume amewaachia waislamu wamchague kiongozi wa mtakaye ambapo wakamchagua Abubakar bin kuhafah  kuwa Khalifa. na Mashia wakasema kuwa mtume aliacha amemchagua atayekuwa kiongozi baada yake ambaye ni Sayyidna Ally bin abi talib na kizazi chake.Mpaka kufika hapa tunaona kuwa mtume na maswahaba ndio msingi na mhimili mkuu wa madhehebu ya Suni.Na kwa upande wa mashia msingi na mhimili wao mkuu ni  mtume na watu wa nyumbani  kwa  mtume (Ahlul bayt a.s).   Na hapa tunaona kuwa madhehebu haya mawili yanashuhudia kuwa: Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hakuzaa wa hakuzaliwa na mtume Muhammad s.a.w ndiye mtume wa mwisho, madhehebu haya pia wanasali sala tano, wanafunga, wana kwenda hijja, wanatoa zaka na wanaamini ufufuo baada ya kifo. Kwa kifupi hakuna shaka kwamba madhehebu haya, yanashikamana na misingi ya dini ya kiislamu kama inavyotakiwa. Lakini  jambo la kusikitisha ni kwamba kadri muda unavyo kwenda ndivyo  madhehebu mapya yanajitokeza na kujipa majina ya kuvutia,wakisambaza fikra potofu na hatimaye kuchafua jina lna kushusha hadhi ya  waislamu na uislam kwa jumla. Madhehebu haya yamewakufurisha kila waliopingana na mitazamo yao na hata kutoa hukumu ya kuawa wapinzani wao, wanafanya haya yoote wakiamini kuwa wenyewe tu, ndio waislamu halisi na madhehebu mengine yoote ni uzushi na upotefu mtupu.    Jambo la kutia moyo ni kwamba Allah ameahidi kuilinda dini yake hata kama jambo hili litawaudhi baadhi ya watu. Kama nilivyo tanguliza kusema hapo juu kuwa madhehebu makuu ni mawili na mengine ni matawi ya madhehebu haya, ningependa kuelezea itikadi na mitazamo za madhehebu haya, lakini kwa kuwa dhehebu la sunni ndio dhehebu lenye wafuasi wengi sana Tanzania na hata Afrika kwa Ujumla, sita lizungumzia dhehebu hili kwakina, bali nitapenda kuelezea dhehebu la Shia au (Ahlul bayt) ili tupate kuwatambua watu hawa.Neno Shia katika lugha ya kiarabu lina maana ya mfuasi.Katika historia neno Shia wametumika kuwaita watu wafuatao:1. Limetumika kuwa ita wanaoitikadia kuwa Sayyidna Alli bin Abii Talib ndiye sahaba bora kuliko masahaba woote.2. Pia linatumika kuwa ita wanaoitikadia kuwa mtume aliacha amemchagua Sayyidna Ally bin abi talib na kizazi chake kuwa ni makhalifa na viongozi wa uislamu baada yake , na wala hakuacha waislamu wafanye uchaguzi wa makhalifa kama ilivyo kwa dhehebu la sunni.Mashia nitaowazungumzia hapa ni mashia kwa maana ya pili ambao kwa jina lingine wanaitwa:  madhehebu ya Ahlul bayt au shia ithna asharia .Hivyo Allah akinipa taufiki, katika mada ifuatayoNitazungumzia dhehebu hili ili liwe wazi kwa woote.