Main Title

source :
Alhamisi

11 Oktoba 2012

20:30:00
355785

tiba na historia yake sehemu ya kwanza Na: Mketo Matenga

Elimu ya Tiba na historia yake katika uislamu

Bismillah Rahmani Rahim Baada ya kumshukuru Mola muumba, nakumtakia rehema na amani mtukufu Mtume(s.a.w.w). Nachukua nafasi hii kuelezea kwa ufupi historia ya tiba kwa sura ya ujumla, na kisha kuangalia mtazamo wa dini ya kiislamu kunako tiba . Swali lipaswalo kujiuliza ni kwamba elimu ya tiba ilianza zama gani? Pia mtazamo wa uislamu kuhusu tiba ni upi? Ndugu msomaji tushirikiane ili kupata majibu mema yatakayo tunufaisha sisi na jamii kwa ujumla

Katika suala hili, Kuna khitilafu baina ya wataalamu na wanahistoria kunako uanzishwaji wa elimu hii (ya tiba)! Ambapo baadhi yao wakadai kwamba mwanzilishaji wa elimu hii ni Nabii Idrisa(a.s).Wengine wakasema kuwa mwanzilishi wake ni:Harmas Lul, na wengine wakainasibisha elimu hii ya tiba na tamaduni za Babel, Yemen, Misri, Fars, Hind, Ugiriki  n.k.Wengine wakasema kuwa elimu ya kidaktari imeanzishwa  na kutambulikana kama sanaa, na  baada ya karne nyingi kupita ikapata mfumo na sura mpya na kuwa  elimu kamili.Ndugu msomaji vyovyote  vile iwavyo elimu ya tiba iko sambamba na kuwepo mwandamu katika sayari hii (ya dunia) kwa sababu magonjwa yanaambatana na maisha ya mwanadamu, hivyo kulikuwa kuna aina mbali mbali za matibabu zilizokuwa zikitumika katika kujiponya.Isipokuwa tiba ya zama hizo ni tofauti na sasa kwa kulinganisha na maendeleo ya zama zele na sasa. Hata hivyo kuna tofauti kati ya tiba ya zama hizo na zama hizi,ukilinganisha mendeleo yaliokuwepo zama hizo na zama za leo  kwa sababu zama za Jalinus(201), Biqrati(277) na Plato (428) elimu ya tiba ilipangiliwa kiufanisi na kitaalamu nasikwamaana ya uwanzilishi wa elimuhi,pia baada ya kudhihiri uislamu udaktari uilipanuka zaidi, nani kwasababu uislamu  unasisitiza utafutaji wa elimu katika nyanja tofauti,pia katika kombi maalumu kama vile tiba na-----Mtume  mtukufu [s.a.w.w] anasema ; elimu ziko ya aina mbili;Elimu ya dini na ya miili. Maendeleo ya tiba yaliboreka kama ifuatavyo  a)Kutoka zama za Mtume mtukufu mpaka mwaka[133 A.H] sawa na[750 A.D]Zama hizi za zinaambatanisha kuanzia zama za uongozi wa Mtume mpaka mpaka zama za makhalifa wanne.Katika zama hizi kwa sababu ya upya wa serekali ya kiislamu zama zile waislamu walishindwa kuipa kipaombele kwa sababu hiyo hakukupatikana daktari aliye bobea katika elimu hii.Isipokuwa kuna watu kadhaa walikifahamika kuwa madaktari wa zama zile kama1-Shimrdel 2-Dhamad bin Thaalabah3-Ibun Abi Ramdhah Tamimi-katika upasuajib)Kutoka mwaka (133A.H)mpaka mwaka (287A.H) sawa na (900A.D)Zama hizi zilifanyika kazi mbili nazo ni kama zifuatazo;1)zama za tarjama:Zama hizi waislamu walianza kutarjum vitabu vya Kigiriki, Kirumi na Kihindi ambae aliyeiongoza kazi hii ni Muheshimiwa Abu Zaidi Husayni bin Is-haka na mwanae.2)Zama za utunzi na uandishi wa vitabu vya tiba ambapo Muheshimiwa Abu Hasan Ally bin Sahari bin Tabariy ambae aliandika kitabu kwa jina Firdawsi al Hikmah, akiwa ni mwandishi wa kwanza katika  elimu ya tiba kwa  waislam.c) kuanzia mwaka (287-700A.H)  ni zama ambazo waislamu walipiga hatua na kuendelea katika taaluma ya tiba kiasi kwamba wasomi wa kimagharibi walisema kuwa muda huu ni: wa thamani na wa dhabu kwa waislamu kimaendeleo.Dokta mmoja miongoni mwa Wamagharibi katika zama ambazo wamagharibi walipokuwa katika kipindi kibaya, kipindi  ambacho waislamu katika miji tofauti ya kitamaduni ulimwenguni wakisonga mbele kimaendeleo ambapo Bagdad, Damaskas, Kairo na miji mengine ambapo mashule ya kidaktari na tiba pia mahospitali kujengwa katika miji hiyo hali ambayo ikionyesha maendeleo ya hali ya juu katika elimu ya tiba na udaktari.Anaendelea kusema kuwa Baghdad zilijengwa hospitali zaidi ya 60 na Kairo 33 hali ya kuwa ndani ya Ulaya hospitali ya kwanza ilijengwa mwaka 1793 (A.D) katika mkoa  wa Yuraki Uengereza.                            Madaktari mashuhuri wa zama hiziKatika zama hizi walipatikana madaktari tofauti miongoni mwao :Ibn Sina, Razi, Ahwazi, Jurjaniy, n.k d)Zama ambazo wailamu walishuka kitaaluma kwa sababu:1 -Kukithiri kwa vita2 –Kukithiri khitilafu za kimadhehebu baina  ya waislamu3 –Kukimbia kwa wanazuoni na kwenda nchi nyengine4 –Kuchomwa moto maktaba za kiislamu Sababu hizi zilipelekea waislamu kuporomoka kielimu na kuwaathiri waislamu.Hivyo baada ya kuporomoka waislamu ndipo nchi za kimagharibi zikaanza kupambamoto na kuanzisha kitengo cha kuhuisha elimu ya tiba katika  karne ya 16 nchini Uengereza mkoa wa  Yurak.Hii ni ishara iyoneshayo kuchelewa kimaendeleo katika nchi za kimagharibi ukilinganisha na wasilamu katika kipindi hicho.*  Misingi  ya tiba na udaktari ulianza pamoja na kuwepo mwanadamu katika sayari hii na kwa kupitia karne mpaka kwenda nyengine elimu hii ikiimarika zaidi na ulipofika uislamu kwa kuwa uislamu unasisitiza kutafuta elimu na kutafakari pia uashiriaji  wa uislamu  kunako aya na hadithi za tiba na udaktari,Waislamu walijiingiza katika elimu hii hatimae kutoa madaktari mfano wa Ibn Sina, baada ya hapo maadui wa uislamu walipora elimu hii na nyengenezo kama elimu ya kemiya  na kujitangaza kuwa wao ndio wenyewe.