Main Title

source :
Jumapili

2 Machi 2014

20:30:00
510804

RAFIKI WA KWELI

Neno hili tumekuwa tukilitumia tangu watoto mpaka hivi sasa, maneno mengine yanayomaanisha neno hili ni pamoja na Swahiba,Shoga,mwanadani, mchizi na nk. Rafiki ni mtu ambaye anaelewana,anapendana na kuaminiana na mwenzake.

Kwa kuwa mwanadamu ni kiumbe anayependa kuishi nawenzake daima amekuwa akihitaji kufanya urafiki na wenzake na hufurahi kuwa na marafiki wenye sifa zinazokubaliana nae. Na kinyume chake ni kwamba mwanadamu huchukia uadui na upweke.    Mwana Falsafa Aristotle anasema kamba: mwanadamu anahitaji rafiki katika hali ya furaha na katika hali huzuni, ili wafurahi pamoja wakati wa furaha na waliwazane wakati wa huzuni.Mwanadamu huwa hajitoshelezi kwa kila kitu, hivyo huitajia kwa wengine pia na hii ndio sababu ya kupatikana jamii yenye mpangilio, umoja na upendo.   Urafiki unatofautiana daraja: kunarafiki wa karibu(Intimate Friend) au mwandani, kuna rafiki wa kawaida na kuna jamaa.Rafiki wa karibu (pal) ni wale ambao tunashirikiana nao katika mengi na maranyingi huwa tunakuwa nao pamoja ima kwa kuonana au kwa kuwasiliana na watu hawa huwa tunawapa hata baadhi ya siri zetu.   Urafiki unatofautiana kutokana na asasi na misingi ya urafiki huo:Kuna unaurafiki unaozingatia asasi ya umri,jinsia, kabila,hobi,michezo, na mengine mengi.  Faida za Marafiki:Marafiki wanafaida nyingi moja kati ya hizo ni: Hukufanya uwe na furaha, na wanaweza kukufaidisha kama watakuwa ni wazuri.Hasara za Marafiki:  Kwa kawaida binadamu huwa wanatabia ya kuathirika na tabia za wapenzi au rafiki zao, hivyo kama rafiki yako atakuwa na tabia mbaya kuna uwezekano mkubwa wa wewe pia kuathirika na tabia hizo.Kama hawatokuwa ni marafki waaminifu wanaweza kutoa siri zako au hata kufanya mbinu za kukudhuru. Kuna watu huwa wanakuja na vazi la urafiki wanamaneno matamu na nasaha za kuvutia, kumbe ni wanafiki wanalengo baya nawe.Maneno ya wanafalsafa na wanafikra kuhusu Marafiki:Ali bin Abitwalib (a.s): “usimwamini sana rafiki na wala usimwamini kabla ya kumpima”.Pia anasema:”katika matatizo hufahamika rafiki wa kweli”.(a friend in need is a friend indeed) Elbert Hubbard “A friend is someone who knows all about you and still loves you.” Abraham Lincoln “Do I not destroy my enemies when I make them my friends?”  Kwamtazamo wako rafiki wa kweli ni nani? acha comment zako katika website yetu ya kielimu ya www.tafakuri.com                                                Tafakari!