Main Title

source :
Ijumaa

14 Machi 2014

20:30:00
514194

sehemu ya kwanza

JE NI KWELI MASHIA HUTUKANA MASWAHABA?

Imekuwa ni tuhuma maarufu na mashuhuri, inayosambazwa na baadhi ya watu kuhusu Mashia, kwamba wanatukana maswahaba, na tuhuma nyingine nyingi. Kabla ya kuichunguza tuhuma hii, kwanza nataka kuweka wazi maana ya kutukana au matusi ili tuweze fahamu je ni kweli maswahaba wanatukanwa

Kutusi ni kusema maneno maalum, ambayo yanakirihi kuyasikia.Nasasa tuchunguzunguze uhalisia wa Maswahaba, ili baadae tuje tfahamu je ni kweli Mashia wanatusi maswahaba?KUHUSU MASWAHABA  Ukweli ni kwamba tunapowaweka maswahaba katika meza ya uchunguzi tunakuta kuwa maswaha hawako nje ya mambo matatu:Kwanza: Maswahaba wote ni waadilifu na watukufu, na kila wanachokisema na kukifanya ni sahihi na wote  wanafaa kufuatwa. Huu ni mtazamo wa Ahlusunna.Pili: Maswahaba ni kama watu wengine, wapo wenye adili na wapo waovu. Vipimo vyao ni matendo yao, wema kwa matendo mema na waovu kwa maovu. Huu ni mtazamo wa Mashia.Tatu:Maswahaba wote ni waovu: Hakuna hata kundi moja katika makundi ya kiislamu yenye itikadi kama hii.  Hizi taswira tunazoweza kuzichora kuhusu maswahaba, hivyo basi hatunabudi kujadili mitazamo hii kwa kina ilikujua ukweli uko wapi,?ama kuhusu jambo la tatu hapana shaka kwamba ni batili na haliamini ila adui wa uislamu.ama jambo la kwanza linawapa maswahaba utukufu usio na kifani na kuwafanya maswahaba kuwa maasumu kama malaika kwa kutofanya kwao dhambi. Mtazamo huu haukubaliwi na uislamu woote, na uko nje ya mafunzo ya kiislamu.   Hivyo tunabaki na mtazamo wa pili ambao ni mtazamo wa kati kwa kati, mtazamo huu ndio itikadi ya Mashia kwa maswahaba: kwamba ubora wa swahaba unatokana na amali zake.    Ikiwa jina swahaba linamaanisha kila aliyemuona mtume na kumfuata au kusikia hadithi zake basi litakuwa linakusanya waumini na wanafiki kwa pamoja ,pia wenye adili na waovu.Kama vile ambavyo mtume s.a.w alivyolitumia neno swahaba katika vita vya Tabuuk pindi alipohabarishwa na Jibril walipokuwa wakitetea wanafiki, waliponena kwamba: Muhammad anajifanya anajua mambo ya minguni ilihali ya duniani hayajui. Baada ya kugundulika walonena hayo Saad bin Ubadah alitaka kuwaua mtume alimkataza akasema:(ni aibu kusikika kuwa Muhammad s.a.w ameua maswahaba wake waache tuishinao kwa wema maadamu wapo pamoja nasi) Dalailu nubuwah kitabu cha Bahiiqii Juzuu:5 uk: 256-257 Hapa tunafahamu kuwa uswahaba sio vazi ambalo ukilivaa unatakasika na kuwa na mtakatifu, bali matendo na amali ndio sababu ya utukufu na adili.Kuna aya nyingi za Qur an tukufu pia hadithi zinazounga mkono mtazamo wa huu.na hata historia pia inathibitisha kwamba, katika maswahaba wapo wema na wapo waovu na pia wapo wenye imani thabiti ambao hawakumuasi mtume katu na hawa ndio wenye daraja ya juu. Na hawa ndio aliowasifu Allah s.w katika Qur an Suratul Fatih :29 akisema: مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا"Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye ni imara mbele ya makafiri, na wenyekuhurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa matawi yake, kisha yakaitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa sawa juu ya shina wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa"Pia hawa ndio waumini waliotajwa na Allah s.w katika suratul Hujraat:15إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ۚ أُولَٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ   Hakika Waumini ni wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio waliosadiki.Na hao ndio ambao Allah s.w ameamuru kuwafuata aliposema katika Surat Tawbah:119 . يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَEnyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.Na  katika aya ya 100 sura hiyohiyo ya Tawbah: وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُNa wale walio tangulia wakawa wa awali katika Wahajirina na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu amewaridhia, nao pia wameridhia; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.Hawa ndio maswahaba wakweli wamtu Muhammad s.a.w je nani atathubutu kuwapinga na kuwashutumu watu wenye sifa kama hizi? Katika mada ijayo tutaelezea aina ya maswahaba wengine, ambao wako kinyume na hawa ili tujue ukweli wa itikadi za Mashia kuhusu Maswahaba na ubatili wa tuhuma wanazotupiwa.