Main Title

source :
Jumamosi

14 Juni 2014

15:40:45
616001

sehemu ya kwanza

Ukweli kuhusu Kifo

Kifo kimekuwa ni gumzo na kitendawili kilichokosa jibu, kitendawili hiki kimekuwa ni gumzo kubwa sana ambalo limewanyima usingizi watu wengi ikiwepo wanafalsafa na watu wa tafakuri.


Kifo kimekuwa ni gumzo na kitendawili kilichokosa jibu, kitendawili hiki kimekuwa ni gumzo kubwa sana ambalo limewanyima usingizi watu wengi ikiwepo wanafalsafa na watu wa tafakuri.

Tatizo kubwa linalopelekea watu hawa kukukosa usingizi ni kutofahamu uhalisia wa kifo, kwani kufahamu tatizo ni hakutua ya kuelekea katika utatuzi.

Mpaka sasa hakuna mtu aliyeweza kukielezea kifo kama kifo bila ya kuelezea uhai, hivyo tunafahamu kwamba ili kufahamu kifo yatupasa kufahamu uhai. Katika vitu vilivyomshangaza SirKatundu katika uchunguzi huu kuhusu kifo ni kwamba kila alipozidi kufanya uchunguzi juu ya kifo ndipo alipozidi kupata kuufahamu umuhimu wa maisha na muda.

HOFU YA KIFO.

Tunapotazama hali ya kimaumbile ya mwanadamu tunakuta kwamba mwanadamu anavitu vya kukinzana katika mwili wake vitu hivi viko vya hiari na viko vilivyo nje ya hiari: kunafuraha na huzuni, kulia na kucheka, na hali nyingine nyingi lakini hali inayomyima raha zaidi mwanadamu ni uoga na uoga mkuu unao msababishia mwanadamu kupata wahaka na mshtuko mkubwa ni uoga wa kifo.

uoaga wa kifo huwaliza hata mashujaa, laitani kama kungekuwa na dawa ya kuzuia kifo basi wanadamu wengi wangefanya juhudi kwa hali na mali kuweza kuipata dawa hiyo kwa thamani yeyote.

Kogopa kifo na kupenda maisha ni hali ya kimaumbile kwani hata Swala humkimbia Simba kwa kuhofia kifo na kulinda uhai wake.

Mwanafikra mchanga Sirkatundu anasema kuwa: Me nadhani kuogopa kifo kunauchungu zaidi hata ya kifo chenyewe.

Wakati wa kukabiliana na kifo hata mashujaa huteteleka, wauwaji siku ya kuuawa kwao ,hulia na kusaga meno:

Sirkatundu katika uchunguzi wake kuhusu kifo anasema kuwa: kuna sababu tatu zinazopelekea watu wengi kuogopa kifo:

1. Kufa peke yako: mwanadamu hufikiria sana kufa peke yake na kuwaacha familia, marafiki, mke, watoto na watu wengine.

2. Uchungu wa kifo: watu wengi huofia kifo kwa kudhani kwamba kifo kinauchungu sana. Na unapomuuliza mtu ungependa ufe kifo gani? Atakujibu kifo cha taratibu kisicho na uchungu wala misukosuko.

3. Kutojua hatima: watu wengi huugopa kifo kwa kuwa hawajui nini kinajiri baada ya kifo, laitani kama watu wangekuwa na yakini kwamba ukifa utakutana na maisha bora kuliko haya basi kila mtu angelitamani kifo na ingekuwa ni ndoto ya kila mtu kufa.

HOFU KWA WAFU:

Moja kati ya vitu vyakushangaza ni kwamba wanadamu situ kwamba wanaogopa mauti, bali wanaogopa maiti pia, ilihali haina hata uwezo wa kunyenyua kidole.

Wajapani,baadhi ya makabila ya Afrika na sehemu nyingine nyingi wanaamini kwamba, baadhi ya matatizo, majanga na mabalaa yanayotokea duniani husababishwa na mizimu(roho za wafu), hivyo hufanya matambiko, maombolezi na kuiomba mizimu isisababishe majanga na madhara kwao.

Katika mada ijayo kama ntapata wasaa nitaelezea mtazamo wa wanafalsafa na watu watafakuri kuhusu kifo ili kuondoa hofu ya kifo katika moyo wako.