Main Title

source : abna.ir
Alhamisi

9 Aprili 2015

10:05:50
682268

Maandamano Marekani ya kupinga ubaguzi dhidi ya wamarekani weusi + Picha

Imekuwa ni matukio ya kawaida kwa wamarekani weusi kunyanyaswa na kubaguliwa huko Marekani.

Askari mzungu wa South Carolina nchini Marekani amesimamishwa kazi baada ya kushitakiwa kwa mauaji ya mwanamume mweusi aliyempiga risasi mara nane mgongoni alipokuwa akitoroka. Mauaji hayo yanayohusishwa na suala la ubaguzi wa rangi yamechochea kwa mara njyingine maandamano Marekani ya kupinga ubaguzi wa rangi unaofanywa na maafisa wa usalama wazungu dhidi ya raia weusi. Mauaji hayo yalitokea siku ya Jumamosi katika mji wa North Charleston na mtu aliyekuwa karibu na eneo la tukio, alirekodi kisa hicho na kuitumia familia ya muathiriwa Walter Scott mwenye umri wa miaka 50 video hiyo inayoonyesha askari Michael Slager mwenye umri wa miaka 33 akimpiga risasi Scott mgongoni alipokuwa akikimbia.

Askari huyo awali kabla ya video hiyo kufichuliwa alikuwa alitunga uongo na kudai kuwa Scott alimnyanganya bastola yake.

Imekuwa ni matukio ya kawaida kwa wamarekani weusi kunyanyaswa na kubaguliwa huko Marekani.