Main Title

source : abna.ir
Jumapili

12 Aprili 2015

18:01:48
683135

Saudi Arabia yaitaka Iran kukoma kuingilia Yemen + Picha

Saudi Arabia imepuuzilia mbali wito kutoka kwa Iran wa kutaka kusitishwa mashambulizi ya anga dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen na kuitaka Iran kutojiingiza katika mzozo huo.

Saudi Arabia imepuuzilia mbali wito kutoka kwa Iran wa kutaka kusitishwa mashambulizi ya anga dhidi ya wananchi madhulumu wa Yemen na kuitaka Iran kutojiingiza katika mzozo huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Saud al Faisal amesema: Iran haiwezi kuitaka kusitisha vita kwani inachojaribu kufanya ni kurejesha utawala halali Yemen wa Rais Abedrabbo Mansour Hadi madarakani ambaye wananchi wa Yemen hawamtaki, jambo lilipelekea kufukuzwa na wananchi hao katika nchi hiyo na kukimbilia Saudia arabia.

Kampeini ya kijeshi inayozishirikisha nchi za ghuba zikiongozwa na Saudi Arabia zimeingia wiki ya tatu tangu kuanza tarehe 26 mwezi uliopita na mapigano makali yameripotiwa hii leo katika mji wa Aden huku Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius ambaye yuko ziarani mjini Riyadh akisema yuko nchini Saudi Arabia kuonyesha nchi yake inaunga mkono juhudi za Saudi Arabia za kurejesha uthabiti Yemen.

Kiongozi mkuu wa Iran ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran Ayatollah Ali Khamenei, amesema inasikitisha sana kwa nchi kama Saudia arabia kusema kuwa Iran inaingilia mambo ya ndani ya Yemen ili hali Saudia arabia ndio imepeleka majeshi na kuivamia Yemen, kwa lengo la kuwaadhibu wananchi mpaka wasalimu amri na kumkubali rais Hadi ambaye ni kibaraka wa Saudia arabia, Marekani na Israel.

Mauaji ya Saudia arabia nchini Yemen