Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

17 Aprili 2015

18:11:31
684466

Kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Daesh auawa Iraq + Picha

Kuawa kwa Izzat Ibrahim al-Douri kunahesabika kuwa ni ushindi mkubwa kwa majeshi ya Iraq ambayo yanapambana na magaidi hao kwa msaada mkubwa kutoka Iran.

Aliyekuwa msaidizi wa karibu wa rais wa zamani wa Iraq, Dikteta Saddam Hussein, Ezzat al-Douri, ameuawa katika operesheni ya kijeshi iliyofanywa na jeshi la Iraq likisaidiwa na wapambanaji wa kishia wanaoungwa mkono na Iran.

Vyombo ya habari nchini Iraq vimeripoti kuwa Izzat Ibrahim al-Douri, ambaye wakati mmoja alikuwa makamu wa Dikteta Saddam Hussein na mmoja wawaanzilishi wa kundi la kigaidi la Daesh Iraq, ameuawa.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Salahuddin. Kituo cha televisheni cha Al-Arabiya kimeonyesha picha za mtu aliyekufa anayefanana na Al-Douri, anayeaminika pia kuhusika na uasi dhidi ya serikali ya sasa ya Iraq inayoongozwa na waislamu wa dhehebu la Shia.

Kuawa kwa Izzat Ibrahim al-Douri kunahesabika kuwa ni ushindi mkubwa kwa majeshi ya Iraq ambayo yanapambana na magaidi hao kwa msaada mkubwa kutoka Iran.