Wakati mwezi mzima umefika tangu Saudia arabia kuanza mashambulizi dhidi ya raia wa Yemen bila mafanikio, serikali ya kifalme ya nchi hiyo imepanga kutuma jeshi maalum ili kupambana na wanaharakati wa kishia wa Huthi na kuwalazimisha wananchi wa Yemen kumrudisha madarakani rais Mansoor Hadi.
Shambulio la anga lililofanywa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya kituo cha usalama kinachoshikiliwa na wanaharakati wa kishia wa Huthi kaskazini magharibi ya Yemen limesababisha vifo vya raia wasioa na hatia takriban 25. Watu waliouwawa walikuwa wakiishi katika jengo karibu na kituo hicho cha usalama ambacho ndio kilicholengwa.
Nae mfalme wa Saudi Arabia Salman leo ameamuru jeshi la ulinzi wa taifa , ambalo linatambulika kuwa na vifaa vya kisasa zaidi nchini humo katika majeshi ya ardhini , kushiriki katika uvamizi wa Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa na kuhakikisha kwamba wananchi hao wanasalimu amri na kumrudisha madarakani rais wasiye mtaka.
Operesheni za kijeshi katika kampeni hiyo hadi sasa zimefanywa na jeshi la anga la Saudi Arabia na jeshi la kawaida nchini humo ambalo linapata amri kutoka wizara ya ulinzi. Jeshi la taifa liko katika mfumo tofauti na lina wizara yake binafsi.
Hatua hii ya kuliagiza jeshi la taifa inakuja baada ya majeshi ya kawaida ya Saudia arabia kushindwa kuingia mpakani mwa Yemen, ambapo katika majaribio ya kuingia Yemen, Saudia arabia ilipata pigo la kumpoteza Jenerali wake mmoja ambaye aliuawa na wapiganaji wa Yemen.
Wakati huo huo shirika la kimataifa la kuwahudumia wahamiaji limesema leo linasitisha kwa muda operesheni ya kuwaondoa wageni kutoka Yemen kwasababu ya vikwazo vya kiusalama vinavyosababishwa na pande zote zinazohusika katika mzozo huo.
IOM imesema imewahamisha zaidi ya raia wa kigeni 400 kutoka katika nchi hiyo inayokumbwa na vita tangu Aprili 12.