Main Title

source : abna.ir
Jumapili

3 Mei 2015

11:56:40
687964

Saudia arabia yatumia mabomu yaliyoharamishwa kimataifa dhidi ya raia wa Yemen + Picha

Saudia arabia imekuwa ikiwashawishi waislamu kwenda kupambana Yemen, kwa kuwalaghai kuwa wanakwenda kupambana jihadi.

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema serikali ya kifalme ya Saudi Arabia imetumia mabomu ya mtawanyo katika uvamizi wake wa mashambulio ya anga dhidi ya raia washiojiweza wa Yemen.

Shirika hilo limeonya hatua hiyo inaweza kuwa na madhara ya muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo.  Mabomu hayo yaliopigwa marufuku ambapo mara nyengine hayaripuki wakati yanapodondoshwa, na badala yake huripuka baadaye na kusababisha maafa makubwa kwa watu wasio na hatia.

 Shirika hilo la Human Rights Watch limesema limekusanya video, picha na ushahidi mwengine unaoonesha mabomu ya mtawanyo yametumiwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika mashambulio yao ya anga dhidi ya wananchi wa Yemen katika  mkoani Saada na eneo la milima kaskazini mwa Yemen.

Pia Saudia arabia imekuwa ikiwashawishi waislamu kwenda kupambana Yemen, kwa kuwalaghai kuwa wanakwenda kupambana jihadi.

Serikali ya Saudia arabia inakabiliwa na mashtaka ya kuzuia misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa vita wa Yemen.