Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

22 Mei 2015

11:01:30
691360

Vyumba maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kiislamu katika mashindano ya kimataifa ya Qur an tukufu Iran + Picha

Katika mahema hayo pia kuna mahema maalum kwa ajili ya ushauri wa mambo mbali mbali yakiwemo ya kiafya, kijamii na kifamilia.

Pamoja na kufanyika mashindano ya kimataifa ya Qur an tukufu katika mji mkuu wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran – Tehran, pembezoni wa ukumbi wa mashindano hayo, kumewekwa vyumba maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo ya dini tukufu ya kiislamu, vyumba hivyo vinafahamika kama “mahema ya Maarifa”.

Katika vyumba hivyo watu mbali mbali wanahudhuria ambapo wanauliza maswali na kujibiwa pia wanapatiwa vitabu mbali mbali vya kiislamu.

Katika mahema hayo pia kuna mahema maalum kwa ajili ya ushauri wa mambo mbali mbali yakiwemo ya kiafya, kijamii na kifamilia.

Pia kuna hema la kituo cha tahakiki za masomo kwa njia ya Computer cha An nur, ambacho kinatoa CD zilizosheheni masomo, vitabu na anuai za tahakiki za kielimu.