Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

22 Mei 2015

18:34:29
691442

Shambulizi la kujitoa mhanga laua watu 10 katika msikiti wa mashia Saudia arabia + Picha

Imekuwa ni ada kwa waislamu wa dhehebu la Sunni wahabia kusambaza chuki dhidi ya waislamu wa Shia na hatimaye kufanya mashambulizi dhidi ya waislamu hao.

Takriban watu 10 wameuawa katika shambulizi la kujitolea muhanga katika msikiti wa waislamu wa dhehebu la Shia katika mkoa wa mashariki wa Saudi Arabia.

Shambulizi hilo limefanywa wakati waumini wa kishia wakiwa katika sala ya Ijumaa.

Daktari wa kukabiliana na dharura katika hospitali ya Qatif amesema kuwa takriban watu sabini wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo lilofanywa dhidi ya mashia wa Saudia arabia.

Walioshuhudia wameripoti mlipuko mkubwa katika msikiti wa Imam Ali uliopo katika kitongoji cha al-Qadeeh, katika jimbo la Qatif Saudia arabia.

Hili ni tukio la kwanza la kigaidi dhidi ya waislamu wa Shia wa Saudia arabia ambao wanatengwa na kunyimwa uhuru na serikali ya Saudia arabia, kiasi ambacho nchi hiyo inashindwa hata kueleza kuwa katika nchi ya Saudia arabia kuna wafuasi wengi wa dhehebu la Shia.

Imekuwa ni ada kwa waislamu wa dhehebu la Sunni wahabia kusambaza chuki dhidi ya waislamu wa Shia na hatimaye kufanya mashambulizi dhidi ya waislamu hao.

Waislamu wa dhehebu la Wahabia au salafia ndio waislamu wengi katika taifa la Saudia arabia wakifuatiwa na waislamu wa Shia na Sunni.