Main Title

source : abna.ir
Jumapili

24 Mei 2015

18:15:12
691824

Washiriki wa mashindano ya kimataifa ya Qur an wakutana na Kiongozi Muadhamu wa mapinduzi ya ya kiislamu ya Iran + Picha

kuitumia Qur an katika nyanja zote za kimaisha binafsi na ya kijamii ya waislamu, na kusisitiza kwamba ili kufikia lengo hili tukufu waislamu wanahitaji wawe na Azma na wawe macho katika kulifikia lengo hili.

 Baada ya kumalizika mashindano haya ya 32 kimataifa ya Qur ani tukufu, ambayo yalikusanya washiriki wa kisomo cha Qur an na washiriki wa kuhifadhi Qur an ambapo katika halfa ya kuhitimisha mashindano hayo Spika wa bunge la Jamhuri ya kiislamu ya Iran, Dk: Ali Larijani alihudhuria katika hafla hiyo na kutoa hotuba pia walihudhuria viongozi wengine wangazi mbali mbali wa serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Baada ya kumalizika masindano washiriki wa mashindano haya wamepata fursa ya kuonana na kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei.

Katika mkutano huo kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei alisisitiza kwamba: Fikra za kuleta tofauti katika uislamu, tofauti kati ya Shia na Sunni, tofauti kati ya waarabu na waajemi, tofauti za mataifa na aina yeyote ya ubaguzi zinatakiwa kupigwa vita.

Mkutano huo umesadifiana na kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Abul Fadhil Abbas ambaye ni mtoto wa Sayyida Ali a.s ambaye ni wasii na khalifa wa mtume Muhammad s.a.w.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Imam Khomein katika jiji la Tehran Iran ambapo mkutano huo ulifunguliwa kwa kisomo cha Qur an tukufu, ambapo wasomi wa Qur ani walioshiriki katika mashindano ya 32 ya kimataifa ya Qur an tukufu, walisoma aya za Qur an tukufu katika hafla hiyo iliyo hudhuriwa na kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei.

kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei katika mkutano huo alisisitiza kuitumia Qur an katika nyanja zote za kimaisha binafsi na ya kijamii ya waislamu, na kusisitiza kwamba ili kufikia lengo hili tukufu waislamu wanahitaji wawe na Azma na wawe macho katika kulifikia lengo hili.

kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei aliendelea kusema kuwa: Dawa na kinga pekee ya matatizo ya ulimwengu wa waislamu ni kujisalimisha kwa sheria na mafunzo ya Qur an tukufu na kutojisalimisha katika fikra za kijahili na potovu na kukabiliana na watu wanaosambaza fikra potofu za kijahili.

kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei alisisitiza kwamba kusoma na kuhifadhi Qur an ni hatua ya kujipamba na tabia na hulka za Qur an na ni sababu ya jamii kuwa jamii yenye kuzingatia mafunzo ya Qur an tukufu.

kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei aliendelea kusema; kwa bahati mbaya sasa hivi umma wa kiislamu umekubwa na udhaifu, ufukara, tofauti na vita vya ndani ambavyo vinatokana na mashindikizo ya tawala za kijahili ambapo njia pekee ya kupambana na matatizo haya ni kushikamana na kuzingatia mafunzo ya Qur an tukufu.

kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei ameashiria kwamba: kama tutajitahidi kupika hatua moja katika kutekeleza mafunzo ya Qur an tukufu, basi Mwenyezi Mungu mtukufu atatupa nguvu mara dufu, haya nayo yasema ni mambo ambayo sisi wairan tumejaribu kuyafanya na tumepambana na mataifa dhalimu na Mwenyezi Mungu mtukufu ametusaidia na kutupa nguvu na uweze mara dufu.

kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei amesisitiza kwamba waislamu na nchi za kiislamu watazame sira na historia jinsi wananchi wa Iran walivyoweza kukabiliana na mataifa yenye nguvu.

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei aliendelea kusisitiza kwamba: mtu yeyeto atayetumia uwezo na sauti yake kusababisha fitna na tofauti katika uislamu anatakiwa afahamu kwamba anawasaidia maadui wa uislamu

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei alisisitiza kwamba: Fikra za kuleta tofauti katika uislamu, tofauti kati ya Shia na Sunni, tofauti kati ya waarabu na waajemi, tofauti za mataifa na aina yeyote ya ubaguzi zinatakiwa kupigwa vita.

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei aliendelea kusema kwamba: Kuwa na uwezo sahihi wa kuchambua na kumtambua Rafiki na Adui ni jambo la muhimusana kwa waislamu.

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei aliendea kusisitiza kwamba: Kwa kutumia elimu na mtazamo wa hali ya juu, kutambua njia sahihi, kukabiliana na matatizo, njama na fitna litakuwa ni jambo jepesi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei aliendelea kusema kuwa: kusoma Qur na kunawapatia watu nguvu na matumaini zaidi, hivyo tunapaswa kuzidisha kuitilia umuhimu Qur an tukufu.

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei alisisitiza kwamba vijana na wanazuoni wanatakiwa kusoma na kutafakari zaidi mafunzo ya Qur an tukufu, kwani kutafakari aya na mafunzo ya Qur an tukufu kuna athari nzuri na matunda mema katika fikra na matendo yetu.

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei ameelezea kuwa: kuzingatia mafunzo ya Qur an tukufu kunaleta bishara njema katika mustakabali.

Sayid Ali Khamenei ameendelea kusisitiza kwamba: kwa bahati nzuri hivi sana tunaona watu wameanza kuitikia wito na kuelekea kwenye mafunzo ya Qur an na uislamu na hii ndio sababu ya kupatikana matukio ya muamko wa kiislamu katika nchi za mbali mbali.

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei aliendelea kusema kuwa huu mwamko na hamasa za kiislamu zinashoshuhudiwa ni hamasa za kweli na haziwezi kuzimwa bali kila siku zitaongezeka na kuzidi kuchukua nafasi mpya.

Kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, Sayid Ali Khamenei katika kumalizia alisisitiza kuwa: Nchi za kiislamu zinatakiwa zitekeleze na kufuata mafunzo ya Qur ani tukufu nasi kuishia kusoma Qur an tu bila ya kufanyia kazi maagizo na mafunzo yake.