Main Title

source : abna.ir
Jumatano

27 Mei 2015

18:40:54
692329

Majeshi ya Yemen yaendelea kujibu mashambulizi ya Saudua arabia + Picha

Majeshi ya Yemen yakishirikiana na wapiganaji wa kikabira yameendelea kufanya hujuma mzito katika vikosi vya jeshi vya mpakani vya Saudia arabia

Majeshi ya Yemen yakishirikiana na wapiganaji wa kikabira yameendelea kufanya hujuma mzito katika vikosi vya jeshi vya mpakani vya Saudia arabia, na kupelekea hasara kubwa kwa majeshi ya Saudia arabia, ambapo wanajeshi wengi wa Saudia arabia wameonekana wakikimbia kambi zao na kurudi  nyuma.

Mkuu wa wanaharakati wa kishia wa Huthi nchini Yemen, amesema wataendelea kufanya mashambulizi nchini Saudia arabia na mashambulizi yao yatafikia mpaka mji mkuu wa Saudia arabia, Riyadh na  miji mingine, lakini hawata lenga miji mitukufu ya kiislamu.

Kwa upande wa pili ndege za kivita za nchi shirika zinazoongozwa na Saud Arabia zimehujumu makao makuu ya wanahatakati wa kishia  wa Huthi katika mji mkuu wa Yemen-Sanaa na kuwauwa wanajeshi 36-mashahidi na maafisa wa afya wamesema. Nchi shirika zinazoongozwa na Saud Arabia zimeanza hujuma zake dhidi ya wananchi wa Yemen wanaompinga rais Hadi ambaye ni mshirika wa karibu wa Marekani na Saudia arabia, mashambulizi ya Saudia arabia dhidi ya wananchi wa Yemen yalianza tangu tarehe 26 mwezi wa 3 mwaka huu wa 2015, kwa lengo la kumrejesha madarakani rais Abedrabbo Mansur Hadi ambaye ni mshirika wao.

 Hujuma za leo zimelenga makao makuu ya uongozi wa vikosi maalum vinavyomtii Ali Abdallah Saleh, kusini mwa Sanaa pamoja pia na ghala ya silaha iliyoko Fajj Attan-karibu na mji mkuu huo. Afisa kutoka wizara ya afya inayodhibitiwa na wanahatakati wa kisia  wa Huthi amesema kwamba wanajeshi 36 na maafisa wa kijeshi wameuliwa na 100 wengine wamejeruhiwa wakati wa shambulio hilo lililopelekea idadi ya waliopoteza maisha yao kuongezeka na kufikia watu 15.Hujuma nyengine za nchi shirika zimeharibu vibaya sana kituo cha jeshi la majini katika mkoa wa Hodeida katika bahari ya Sham.

wanahatakati wa kisia  wa Huthi na majeshi ya Yemen yamefanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya Yemen na kuwaondoa magaidi wa Alqaida na Daesh ambao wanatumiwa na Saudia arabia kupambana ili kumrudisha rais Hadi madarakani.

Mauji ya Saudia arabia Yemen