Main Title

source : abna.ir
Jumamosi

6 Juni 2015

19:45:13
694075

Wakurdi waomboleza vifo vya wafuasi wake wawili waliouawa katika mkutano wa kisiasa Uturuki + Picha

Wakurdi nchini Uturuki wamekusanyika kuomboleza na kuandamana mahali palipotokea shambulio la bomu lililosababisha mauaji ya watu wawili na kwajeruhi zaidi ya watu 200 katika mkutano wa kisiasa

Wakurdi nchini Uturuki wamekusanyika kuomboleza na kuandamana mahali palipotokea shambulio la bomu lililosababisha mauaji ya watu wawili na kwajeruhi zaidi ya watu 200 katika mkutano wa kisiasa, huku wengi wakielezea hasira zao kwa rais Tayyip Erdogan juu ya tukio hilo hii ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi wa bunge nchini humo. Miripuko hiyo miwili ambayo rais Erdogan ameitaja kama uchokozi ulionuiwa kusambaratisha uchaguzi wa bunge ilitokea katika mkutano wa chama cha HDP Kusini Mashariki mwa nchi hiyo. Hata hivyo maafisa wa usalama wamesema bado hawajafanikiwa kujua nani aliyepanga shambulio hilo.