Main Title

source : abna.ir
Alhamisi

26 Novemba 2015

19:05:37
721740

Uturuki yashindwa kujitetea na kudai kuwa haikujua kama ndege iliyodunuliwaa ilikuwa ni ya Urusi/ Urusi yaipa harasa kubwa Uturu

Wakati hayo yanajiri ndege za kivita za Urusi zimeshambulia magari Uturuki yaliyosheheni silaha zilizokua zinapelekwa kwa magaidi nchini Syria.

Uturuki yashindwa kujitetea na kudai kuwa haikujua kama ndege iliyodunuliwaa ilikuwa ni ya Urusi/ Urusi yaipa harasa kubwa Uturuki

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Viongozi wa Uturuki baada ya kujisifu na kutangaza kuwa wameidungua ndege ya Urusi, sasa wameamua kubadilisha kauli na kusema kuwa hawakujua kama ndege hiyo ilikuwa ni ya Urusi.

Viongozi hao licha ya kusema hayo wamepinga kabisa kuomba msamaha kwa Urusi na badala yake viongozi wa nchi hiyo wamesema kuwa Urusi isitoe maamuzi kwa kutumia hisia bali itumie maamuzi ya kidimplomasia.

Urusi imesitisha sehemu kubwa ya mahusiano ya kiuchumi na kijeshi kati yake na Uturuki, na imetoa amri kwa wanajeshi wake kuangamiza kitu chochote kitacho ashiria hatari kwa wanajeshi wa Urusi.

Rais Putin wa Urusi ameikosoa vikali Uturuki kwa kudungua ndege hiyo ambayo haikuwa na lengo la kuishambulia Uturuki, na baada ya kuidungua ndege hiyo Uturuki ilikimbilia kutoa taarifa kwa Marekani na NATO ili kupata msaada kana kwamba Urusi ndio imedungua ndege ya Uturuki.

Serikali ya Urusi imeahidi kuwa majibu ya Urusi kwa tukio hilo yatakuwa ni makali na yataleta hasara kubwa kwa Uturuki.

Urusi pia imesema Uturuki imedungua ndege hiyo ikiwa katika  kilometa 4 ndani ya anga la Syria, Urusi imeituhumu serikali ya Uturuki kwa kununua mafuta kwa magaidi wa Daesh na bidhaa zinazoporwa na magaidi hao kutoka Syria.

Urusi imeituhumu serikali ya Uturuki na washirika wake kwa kuwasaidia magaidi nchini Syria.

Jambo la kustaajabisha ni pale rais wa Uturuki alipopinga tuhuma hizo na kusema kuwa serikali ya Syria ndio inayowasaidia magaidi hao.

Urusi imesema inasubiri  jibu linalostahili kutoka Uturuki, kueleza vipi iliidungua ndege ya kivita ya Urusi mapema wiki hii. Msemaji wa Ikulu  ya Kremlin mjini Moscow   Dmitry Peskov aliwaambia wandishi habari kwamba Urusi pamoja na hayo  haina azma ya kuiwekea  vikwazo Uturuki au kuzuia bidhaa za chakula kutoka nchi hiyo.

Hapo mapema wizara ya  kilimo ya Urusi ilitangaza kwamba itaimarisha ukaguzi wa  bidhaa za chakula na kilimo zinazoingia kutoka Uturuki.

Wakati hayo yanajiri ndege za kivita za Urusi zimeshambulia magari Uturuki  yaliyosheheni silaha zilizokua zinapelekwa kwa magaidi nchini Syria.

 

Mwisho wa habari/ 291