Main Title

source : abna.ir
Ijumaa

27 Novemba 2015

16:17:47
721852

Mpalestina awagonga kwa gari wanajeshi wa Israel baada ya ndugu yake kupigwa risasi + Picha

Mpalestina huyo ni Fadi Hassib, kutoka Ramallah, ambaye kaka yake aliuawa kinyama kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel siku ya Jumapili.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mpalestina mmoja amemgonga kwa gari wanajeshi wa Israel katika kituo cha basi kwenye Ukingo wa Magharibi, kabla naye kuuawa kwa kupigwa risasi.

Polisi imesema kuwa gari la Mpalestina huyo liliwagonga wanajeshi wawili wa Israel waliokuwa wamesimama katika kituo cha basi karibu na Kfar Adumim.

Shirika la matibabu ya dharura la Israel, Magen David Adom, limesema kuwa wanajeshi hao wawili walipelekwa katika hospitali ya Jerusalem wakiwa na fahamu zao pamoja na majeraha madogo. Polisi imemtaja Mpalestina huyo kuwa ni Fadi Hassib, kutoka Ramallah, ambaye kaka yake aliuawa kinyama kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel siku ya Jumapili.

Tukio la leo limeifanya idadi ya Wapelstina waliouawa na majeshi ya Israel tangu mwezi Oktoba Mosi, kufikia 98, akiwemo Muisraeli mmoja mwenye asili ya Kiarabu.

Mwisho wa habari/ 291